ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, May 18, 2026

FIRST LAKE VICTORIA DAY KUFANYIKA MWANZA WAZIRI MKUU NDIYE MGENI RASMI

 Maadhimisho ya Siku ya Ziwa Victoria 2026 yanakuja kwa kishindo jijini Mwanza kuanzia tarehe 18 hadi 21 Mei 2026!

Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda ambaye alipata kuzungumza na vyombo mbalimbali vya habari amesema kuanzia tarehe 18 Mei 2026 Kutakuwa na: - Upandaji miti - Uhamasishaji wa utunzaji wa maji - Jukwaa la wadau - Uzinduzi wa Kituo cha Kikanda cha Utafutaji na Uokoaji - Maonesho makubwa ya biashara, huduma na bidhaa mbalimbali katika viwanja vya Nanenane Nyamhongolo.

Nchi mbalimbali za Afrika Mashariki na Ukanda wa Ziwa Victoria zitashiriki pamoja na Tanzania kuwa mwenyeji. Kauli mbiu: "𝗠𝗔𝗝𝗜 𝗬𝗘𝗧𝗨, 𝗠𝗨𝗦𝗧𝗔𝗞𝗔𝗕𝗔𝗟𝗜 𝗪𝗘𝗧𝗨: 𝗧𝗨𝗨𝗡𝗚𝗔𝗡𝗘 𝗞𝗪𝗔 𝗨𝗘𝗡𝗗𝗘𝗟𝗘𝗩𝗨 𝗪𝗔 𝗕𝗢𝗡𝗗𝗘 𝗟𝗔 𝗭𝗜𝗪𝗔 𝗩𝗜𝗖𝗧𝗢𝗥𝗜𝗔” . 📍 Mwanza ndiyo mahali pake!
#LakeVictoriaDay2026 #Mwanza #ZiwaVictoria #Tanzania #EastAfrica Environment Nyamhongolo VictoriaLake

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment