Na Albert G. Sengo | Mwanza
Katika juhudi za kuimarisha uchumi jumuishi na kukuza ujasiriamali miongoni mwa wanawake, Benki ya Akiba (Akiba Commercial Bank) imeendelea kujenga ukaribu wa karibu na wateja wake kupitia mikutano ya moja kwa moja. Moja ya hatua hizo ni mkutano maalum uliowakutanisha akinamama wajasiriamali wa Mwanza, uliofanyika tarehe 31 Machi 2026 katika ukumbi wa ARCH Mayala, Nyakahoja.
Tukio hilo lilihudhuriwa na zaidi ya washiriki 100, wengi wao wakiwa ni akinamama wanaojishughulisha na biashara ndogo na za kati katika maeneo mbalimbali ya Kanda ya Ziwa Victoria kuanzia biashara za vyakula, usindikaji wa mazao ya kilimo, uuzaji wa samaki, hadi huduma za kijamii kama elimu na urembo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment