NA ALBERT G. SENGO/MWANZA
Serikali ya Tanzania imewekeza zaidi ya shilingi trilioni moja katika kuimarisha sekta ya usafiri wa majini nchini, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo pamoja na kukuza uchumi wa Taifa.
Hayo yameelezwa na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa wakati akizungumza na vyombo vya habari jijini Mwanza, ambapo amesema uwekezaji huo umehusisha ununuzi wa meli mpya, ukarabati wa meli zilizopo pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya bandari katika maziwa makuu na ukanda wa Bahari ya Hindi.
Amesema hatua hizo zinalenga kuongeza usalama wa usafiri majini, kurahisisha usafirishaji wa mizigo na abiria, pamoja na kuimarisha biashara kati ya Tanzania na nchi jirani.
Msigwa amesema miongoni mwa mafanikio ya uwekezaji huo ni kuanza kwa huduma za meli ya MV Mwanza, ambayo ina uwezo wa kubeba abiria 1,200, tani 400 za mizigo pamoja na magari makubwa matatu na magari madogo 20.
Ameeleza kuwa Serikali pia inaendelea na ukarabati wa meli ya MV Umoja pamoja na meli ya MT Ukerewe, huku ikiendelea na ujenzi wa meli mpya ya mizigo yenye uwezo wa kubeba tani 3,000 katika Lake Victoria.
Katika Lake Tanganyika, Serikali inaendelea na ukarabati wa meli ya MV Liemba ili kuboresha huduma za usafiri kwa wakazi wa maeneo ya mwambao na nchi jirani.
Mbali na miradi hiyo, Serikali pia inaendelea kuboresha bandari mbalimbali katika maziwa makuu, kujenga bandari mpya pamoja na kuimarisha mifumo ya uokoaji majini kwa kujenga vituo vya utafutaji na uokoaji na kununua boti maalum za uokoaji.
.png)
Msigwa amesema hatua hizo zinaonyesha dhamira ya Serikali ya kuifanya sekta ya usafiri wa majini kuwa ya kisasa, salama na yenye mchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi wa Taifa.
Tupe maoni yako
.png)
.png)
0 comments:
Post a Comment