ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, March 23, 2026

MV LIEMBA MELI YENYE HISTORIA DUNIANI ZAIDI YA MIAKA 100 YAKARABATIWA KWAAJILI YA USAFIRI NA UTALII

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

Meli kongwe zaidi inayobaki duniani na bado inaendelea kutoa huduma, MV Liemba, yenye umri wa zaidi ya miaka 100, inaendelea kufanyiwa ukarabati mkubwa unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 32. Uamuzi wa kuikarabati umetokana na tathmini iliyoonesha kuwa kujenga meli mpya kungehitaji zaidi ya shilingi bilioni 80. Kutokana na umuhimu wake wa kihistoria na kiuchumi, Serikali ya Tanzania imechagua kuirudishia uhai meli hiyo ili iendelee kutumika katika usafiri na usafirishaji katika Ziwa Tanganyika, huku pia ikibaki kuwa kivutio muhimu cha historia na utalii. Akizungumza kuhusu umuhimu wa meli hiyo mbele ya vyombo vya habari jijini Mwanza, Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema kuwa MV Liemba ni hazina ya kipekee duniani, akibainisha kuwa watu kutoka nchi mbalimbali na hata mabara tofauti husafiri kuja kuiona. "Watu wanasafiri kutoka nchi za mbali na mabara tofauti kuja tu kuiangalia meli hii ambayo, licha ya kuwa na umri wa zaidi ya karne moja, bado inaendelea kutoa huduma," amesema. #mvliemba #samiasuluhuhassan #GersonMsigwa #tanzania

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment