BODI ya Rufaa ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) imeivua Senegal ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) na kuwapa wenyeji, Morocco.
Senegal ilitawazwa kuwa bingwa wa AFCON ya 2025 baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Morocco Januari 18, mwaka huu bao pekee la kiungo wa ulinzi, Pape Alassane Gueye anayechezea Villarreal ya Hispania dakika ya 94 katika mchezo uliodumu kwa dakika 120 Uwanja wa Prince Moulay Abdellah Jijini Rabat.
Hata hivyo, CAF imesema kwamba Senegal imepoteza mechi hiyo na Morocco wamepewa ushindi wa mabao 3-0 kwa kutumia Kifungu cha 84 cha Kanuni za AFCON kwa kitendo chao cha kuondoka uwanjani kupinga Penalti waliyopewa Morocco na kusababisha mchezo kusima akwa dakika 14, kabla ya kurejea kumalizia.
Mshambuliaji Brahim Díaz wa Morocco ambaye yeye mwenyewe alichezewa rafu na beki wa Senegal, El Hadji Malick Diouf – alikwenda kupiga penalti kwa staili ya Panenka bahati mbaya ikaokolewa na kipa Édouard Mendy na kuzima ndoto za Simba wa Atlasi kutwaa taji kwa jasho uwanjani.
Tupe maoni yako

0 comments:
Post a Comment