ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, February 21, 2026

SONGORO MARINE UBORA WA KIMATAIFA UJENZI MELI


Kampuni ya kizawa ya Songoro Marine iliyojikita katika ujenzi wa meli ndani na nje ya Tanzania inatajwa ni kampuni inayojenga meli kwa viwango vya kimataifa.


Kampuni hiyo, imekuwa ikipewa zabuni na serikali za ujenzi wa vivuko, kutokana na kuonyesha uzalendo katika kutekeleza miradi kwa viwango vya kimataifa.


Kwa miaka zaidi ya 30 Tangu kuanza kwa kampuni hii ya kizalendo imeonyesha dira kwa kampuni za kizawa baada ya kuaminiwa na serikali katika ujenzi wa vivuko.


Kampuni hii iliyoanza kazi mwaka 1993 kwa sasa imeendeleza mizizi ya ujenzi wa meli za kisasa zinazotumiwa ziwani na baharini kwa kufungua matawi nje ya mipaka ya Tanzania.


Inaelezwa kuanza kufungua matawi nje ya mipaka ya Tanzania ni hatua iliyotokana na kazi iliyotukuka kwa kujenga meli na vivuko vya umma na binafsi kwa viwango vya kimataifa.


Serikali ya Tanzania mara kwa mara imekuwa ikitangaza zabuni za ujenzi wa meli, ambapo kampuni hii ya kizalendo imekuwa ikiibuka kidedea.


Songoro Marine yenye makao makuu yake Ilemela mkoani Mwanza, kwa sasa inaendelea na ujenzi wa Meli tano ambazo zipo katika hatua mbalimbali.


Kati ya hizo meli tano, Meli ya Mv. Ukerewe ambayo imekamilika kwa asilimia 99 itakuwa inafanya safari zake kati ya Rugezi - Kisorya.


Kampuni ya Songoro Marine imekuwa ni mkombozi kwa Taifa kutokana na kujikita katika ujenzi wa meli na kuipa Taifa sofa nje ya Tanzania baada ya nchi ya Uganda kuipa kazi ha ujenzi wa meli.


Songoro Marine yenye tawi lingine, jijini Dar es Salaam ambako ujenzi wa vivuko inaendelea kwa kasi na viwango vinavyohitaji kulingana na mamlaka zinazosimamia sekta hiyo.


Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo, Meja Songoro, Mratibu miradi wa Songoro, Hawa Isakiya, amesema kampuni hiyo imekuwa ikishirikiana na serikali katika ujenzi wa vivuko.


Anasema serikali kupitia  Wakala wa Ufundi na Umeme - Temesa, asilimia 75-80 kazi nyingi wanazofanya na za Umma, ambapo kazi chache zilizobaki ni kutoka nje ya nchi na watu binafsi.


Isakiya anasema kukuwa kwa kampuni wamefanikiwa kuongeza wigo kwa kufungua  tawi lingine nchini Uganda kwa ajili ya kusogeza huduma karibu.


Anaeleza mafanikio hayo yamesababishwa na serikali ya Tanzania kwa kujali wawekezaji wazawa kwa kuwapa nafasi ya kuonyesha uwezo wao.


Isakiya amesema, “kampuni kwa sasa inaendelea na vivuko vingine vinne, ikiwemo Kivuko cha Kome kitakachofanya safari zake Nyakalilo - Kome, Kivuko cha Mv. Bukondo kitafanya safari Bwiro - Bukondo ambacho kipo asilimia 99,”.


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment