NA ALBERT G. SENGO/MWANZA
Mwanza ni kitovu cha uchumi katika Kanda ya Ziwa. Shughuli kuu za uchumi wetu ni pamoja na uvuvi katika Ziwa Victoria, biashara ndogo na za kati, kilimo cha pamba na mazao ya chakula, uchimbaji wa madini, pamoja na sekta ya huduma na utalii.
Kwa wavuvi wanaofanya kazi katika mwambao wa Ziwa Victoria, mawasiliano ya uhakika yanarahisisha biashara ya samaki, kupanga masoko, na kufanya malipo kwa njia ya kidijitali.
Kwa wafanyabiashara wa masoko kama Soko Kuu la Mwanza, Soko kuu la Samaki Kirumba na maeneo mengine huduma za Airtel Money zinarahisisha miamala, kupokea malipo, na hata kuagiza bidhaa kutoka maeneo mengine ya nchi.
Kwa wakulima wa pamba na mpunga katika wilaya za mkoa wa Mwanza, huduma za mawasiliano zinawaunganisha na masoko na taasisi za kifedha.
Hivyo basi, uwekezaji huu wa Airtel Tanzania unaenda moja kwa moja kuunga mkono shughuli hizi muhimu za kiuchumi zinazofanywa na serikali
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment