ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, January 6, 2026

KWANINI MADURI ALIFUNGWA MACHO NA KUZIBWA MASIKIO ALIPOKAMATWA

 .

Picha ya kwanza ya Nicolás Maduro baada ya kuzuiliwa katika operesheni ya kijeshi ya Marekani Jumamosi hii itasalia katika kumbukumbu ya wengi.

Rekodi hiyo ya picha ilitolewa saa chache baada ya wanajeshi wa Marekani kumkamata mtu ambaye alikuwa kiongozi wa serikali ya Venezuela tangu 2013, katika operesheni iliyoamriwa na Donald Trump mwenyewe.

Ni Trump mwenyewe aliyechapisha picha ya Maduro kwenye mtandao wa Truth Social network, wakati ambapo Makamu wa Rais wa Venezuela wakati huo, Delcy Rodríguez, alikuwa akiuliza uthibitisho wa maisha baada ya kukamatwa kwa rais na mkewe.

Kufikia sasa inajulikana kuwa Maduro na mkewe, Cilia Flores, walikamatwa asubuhi na mapema huko Fort Tiuna, kusini-magharibi mwa Caracas, na kisha wakahamishwa kwa helikopta hadi kwenye meli ya kivita ya Iwo Jima ili kupelekwa -kupitia Cuba- hadi New York

Huko, wote wawili wameshtakiwa kwa tuhuma za kula njama za kutumia dawa za kulevya, kula njama ya kuingiza cocaine nchini Marekani, na makosa mengine yanayohusiana na silaha.

Katika BBC Mundo tulishauriana na wataalamu wa ulinzi na operesheni za kijeshi kuhusu hitimisho linaloweza kutolewa kutokana na picha hiyo ya kwanza ambayo Maduro anaonekana akiwa amevalia mavazi ya michezo, huku mikono yake ikiwa imefungwa pingu na huku hisi zake, kama vile kuona na kusikia, zikiwa zimezibwa.

Mbinu za Kawaida

Kwa Mark Cancian, kanali mstaafu wa Jeshi la Wanamaji la Marekani na mshauri mkuu wa Idara ya Ulinzi na Usalama katika Kituo cha Mafunzo ya Kimkakati na Kimataifa (CSIS), "serikali imechukulia kukamatwa huku kama suala la utekelezaji wa sheria, sio operesheni ya kijeshi, kwa hivyo wamemchukulia Maduro kama mfungwa."

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment