ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, January 5, 2026

REFA AINYIMA WAZIWAZI PENATI TAIFA STARS IKITOLEWA AFCON 1-0 NA MOROCCO

 


SAFARI ya Tanzania katika Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 imeishia Hatua ya 16 Bora baada ya kutolewa na wenyeji, Morocco JANA jioni.

Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Prince Moulay Abdellah, Jijini Rabat, Morocco, bao pekee lilifungwa na winga wa Real Madrid, Brahim Díaz, dakika ya 64.

Kocha wa Taifa Stars, Miguel Angel Gamondi, na kikosi chake wameonesha kutoridhishwa na maamuzi ya refa Boubou Traore kutoka Mali, wakidai walinyimwa penalti ya wazi baada ya Iddi Suleiman ‘Nado’ kuangushwa ndani ya eneo la hatari dakika za lala salama.

Morocco sasa inaingia robo fainali na kukutana na Cameroon, waliowaondoa Afrika Kusini kwa ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa usiku kwenye uwanja huo huo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment