TIA Yasistiza Utafiti na Ubunifu Katika Kuchochea Uchumi – Kongamano la Kimataifa la 4 la Usimamizi wa Biashara na Ukuaji wa Uchumi Lafana Mwanza
Mwanza, 25 Novemba 2025 – Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) leo imeongoza Kongamano la 4 la Kimataifa la Usimamizi wa Biashara na Ukuaji wa Uchumi, lililofanyika katika Ukumbi wa Nyerere, Gold Crest Hotel jijini Mwanza, likiwa na ujumbe mahsusi unaoangazia nafasi ya ubunifu, uvumbuzi na biashara katika kuchochea uchumi endelevu.
Akizungumza kumwakilisha mgeni Rasmi, Benjamin Magai ambaye ni Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali , amesisitiza umuhimu wa kuwekeza katika utafiti wa kisayansi, kama njia ya kutoa suluhisho la changamoto za kijamii na kiuchumi. Akibainisha kuwa utafiti ndio injini ya maendeleo, hasa katika maeneo kama ubunifu, teknolojia, tathmini, miundombinu na mikakati ya maendeleo yenye tija.
Dira ya Maendeleo ya 2050 Yawekwa 
Dhima: Uvumbuzi, Ubunifu na Biashara kwa Uchumi Endelevu
Kongamano la mwaka huu limebeba kaulimbiu “Uvumbuzi, Ubunifu na Biashara kwa Uchumi Endelevu.” Kaulimbiu hiyo imegawanywa katika mada 11, huku machapisho 41 ya tafiti yakitarajiwa kuwasilishwa.
Prof. Pallangyo alisema kuwa kabla ya mawasilisho ya tafiti, kutakuwa na watoa mada wakuu 8 (Keynote Speakers) kutoka ndani na nje ya Tanzania, ambao ni wabobezi katika nyanja zao. Miongoni mwao ni:
Watoa Mada Wakuu ni kama ifuatavyo:-
Katika hotuba yake ya ufunguzi, Afisa Mtendaji Mkuu wa TIA, Prof. William Amos Pallangyo, amekumbusha kuwa TIA ni mojawapo ya taasisi kongwe na muhimu nchini katika kutoa elimu ya uhasibu, ugavi na fani nyingine za biashara. Ikiwa na kampasi 8 nchini na zaidi ya wanafunzi 32,000, na taasisi hiyo imeendelea kuimarisha mfumo wa mafunzo unaozingatia umahiri (Competence Based Training – CBET), sambamba na kufanya tafiti na kutoa ushauri wa kitaalam.
Baada ya mawasilisho ya tafiti, TIA imetangaza kuwa itachapisha kitabu maalum kitakachokusanya mapendekezo ya watafiti juu ya namna bora ya kutatua changamoto katika sekta za biashara na uchumi. Kitabu hicho kitasambazwa kwa wadau muhimu, ikiwemo Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kama mchango wa TIA katika kusaidia sera na maamuzi ya maendeleo.
Katika kuunga mkono juhudi za Serikali kukuza utalii, washiriki wa kongamano wamepangiwa kutembelea vivutio vya Jiji la Mwanza. Hii ni sehemu ya mkakati wa kutumia kongamano kama nyenzo ya kuhamasisha utalii wa ndani.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment