ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, May 5, 2025

DR. JEMBE AFAFANUA KWANINI WEMA HAWANA MAISHA - ASHIRIKI MAZISHI YA MWANAMKE KINARA MWANZA

 "Mama Katua ameishi kama kitabu, Hadithi nzuri ambayo imeishia kwenye masikitiko majonzi na huzuni kubwa. Mwanza nzima imemiminika hapa ikionyesha kuguswa na hili" anasema Mkurugenzi wa Jembe Media LTD, Dr. Sebastian Ndege ambaye pia ni CEO wa makampuni ya Ndege Insurance na Jembe Development.

KWENYE MAHOJIANO:- Dr Jembe - "Ngoja Niwape siri, Kuna watu kwenye Maisha ni wema mno na hawana mbadala naye Mungu akiona mnawapenda saaana ndiyo huwa anaondoka nao, mpaka wakati mwingine najionya nisiwe mwema sana" Mwandishi PK - "Ili usife" Dr Jembe - "Eeeeeeh" ..........Kisha wote wakacheka.........!!! Dr Jembe - "Kwasababu wengi wanaofanya wema sana Mungu anaondoka nao, sijui huwa ni nini hicho?" " Kwahiyo ndiyo maana wakati mwingine huwa naamua kuwa mkaksi..... ili niendelee kuwepo" " Lakini yote kwayote mapenzi ya Mungu lazima tuyakubali na nikisema hivi siyo tusitendeane wema la hasha..... watu wema wana faida,tuishi nao na kuwashikilia kwani ukiwapoteza we ndio mwenye hasara... Jifunze kutunza watu hao" MTANGAZAJI :- PASCHAL KADUSHI MAANDISHI :- ALBERT G. SENGO

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.