Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis alifariki dunia Jumatatu ya Pasaka, Aprili 21, 2025, akiwa na umri wa miaka 88 katika makazi yake katika Casa Santa Marta, Vatican.
Taarifa zilizotoka mapema leo, Mwadhama, Kardinali Farrell, alitangaza kwa masikitiko kifo cha Baba Mtakatifu Francis, kwa maneno haya:
"Ndugu wapendwa, kwa huzuni kubwa sina budi kutangaza kifo cha Baba Mtakatifu Francisko''.
Farrell anaongeza: "Kwa shukrani nyingi sana kwa ajili ya kielelezo chake kama mfuasi wa kweli wa Bwana Yesu, tunaipongeza roho ya Papa Francisko kwa upendo wa huruma usio na kikomo wa Mungu Mmoja na wa Utatu."
Kifo cha Papa kimekuja chini ya saa 24 baada ya kujitokeza kwenye Uwanja wa St Peter's Square mjini Vatican kwa ajili ya Jumapili ya Pasaka.
Alitoka akiwa kwenye kiti cha magurudumu na kupunga mkono kutoka kwenye baraza ya Basilica ya St Peter's kwa umati wa watu waliokuwa wakishangilia na kusema: "Ndugu wapendwa, Pasaka njema."
Hotuba yake ya Pasaka na baraka ilisomwa na msaidizi alipokuwa ameketi, akitazama.
Baada ya baraka, alizungushwa kwenye uwanja. Alipopita katikati ya umati, msafara wake ulisimama mara kadhaa huku watoto wachanga wakiletwa ili awabariki.
Katika miezi ya mwisho ya maisha yake, hali mbaya ya afya ya Papa ilimfanya kutumia wiki kadhaa hospitalini.
Mnamo tarehe 14 Februari, mzee huyo wa miaka 88 alipelekwa katika hospitali ya Gemelli huko Roma kutibiwa homa ya mapafu. Alikuwa na shida ya kupumua kwa siku kadhaa.
Aliruhusiwa kutoka hospitali mnamo Machi 23.
Papa alishambuliwa haswa na homa ya mapafu, ambayo ni maambukizi ya ambayo yanaweza kusababishwa na bakteria, virusi au fangasi, baada ya kuondolewa sehemu ya mapafu akiwa kijana.
"Alitufundisha kuishi maadili ya Injili kwa uaminifu, ujasiri na upendo wa ulimwengu wote, hasa kwa ajili ya maskini zaidi na waliotengwa zaidi."
Katika miezi ya mwisho ya maisha yake, hali mbaya ya afya ya Papa ilimfanya kutumia wiki kadhaa hospitalini.
Mnamo tarehe 14 Februari, mzee huyo wa miaka 88 alipelekwa katika hospitali ya Gemelli huko Roma kutibiwa homa ya mapafu. Alikuwa na shida ya kupumua kwa siku kadhaa.
Aliruhusiwa kutoka hospitali mnamo Machi 23.
Papa alishambuliwa haswa na homa ya mapafu, ambayo ni maambukizi ya ambayo yanaweza kusababishwa na bakteria, virusi au fangasi, baada ya kuondolewa sehemu ya mapafu akiwa kijana.
Viongozi mbalimbali wametoa salamu za rambirambi
Rais Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za pole kufuatia taarifa za kifo cha Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis, akisema dunia imempoteza kiongozi wa kiroho aliyeacha alama ya amani, upendo na maendeleo ya watu.
Katika taarifa yake aliyochapisha leo Jumatatu Aprili 21, 2025 katika kurasa zake za mitandao ya kijamii, amesema kwa kipindi cha miaka 12 ya uongozi wake, Papa Francis ameishi kama mwalimu na kiongozi aliyesimamia misingi ya utu, ustawi wa jamii na mshikamano wa kidini.
“Kwa niaba ya Serikali na wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ninatuma salamu za pole kwa waumini wote wa Kanisa Katoliki hapa nchini na duniani kote,” amesema Rais Samia.
Amesema mchango wa Papa Francisko katika kudumisha amani na kuhimiza maendeleo ya binadamu utabaki kuwa kumbukumbu ya kudumu kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
“Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema Peponi,” ameongeza Rais Samia.
Papa Francisko, ambaye alikuwa Papa wa 266 wa Kanisa Katoliki, amefariki dunia leo Jumatatu akiwa na umri wa miaka 88.
Ikulu ya White House imetoa salamu za rambirambi kwa kifo cha Papa katika chapisho kwenye mtandao wa X.
"Pumzika kwa Amani, Papa Francis," chapisho hilo linasema, pamoja na picha ya Papa akikutana na Rais wa Marekani Donald Trump na mkewe Melania, na picha nyingine ya Papa akikutana na JD Vance jana.
Rais wa Tume ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen anasema "aliongoza mamilioni, mbali zaidi ya Kanisa Katoliki, kwa unyenyekevu na upendo wake safi kwa wasiojiweza"
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi anasema "ameumizwa sana" na kifo cha Papa Francis.
Waziri Mkuu wa Poland Donald Tusk anamkumbuka Papa Francis kama "mtu mzuri na mchangamfu "
Rais wa Misri Abdul Fattah al-Sisi anasema Papa Francis "alikuwa sauti ya amani, upendo na huruma"
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.