MABINGWA watetezi, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati mkoani Manyara.
Mabao ya Yanga yamefungwa na mshambuliaji wake nyota, Clement Francis Mzize mawili dakika ya 39 na 70 na viungo, Mburkinabe Stephane Aziz Ki dakika ya 43 na Mzambia, Clatous Chota Chama dakika ya 89.
Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 70 katika mchezo wa 26 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi 13 zaidi ya watani, Simba ambao hata hivyo wana mechi nne mkononi.
Kwa upande wao Fountain Gate baada ya kupoteza mchezo wa leo wanabaki na pointi zao 29 za mechi 27 sasa nafasi ya 11.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.