VICTOR MASANGU/KIBAHA
Katibu wa Nec Itakadi Uenezi na mafunzo wa chama cha mapinduzi (CCM) Taifa CPA Amos Makala amekemea vikali vitendo vya baadhi ya Viongozi na Kamati za siasa ngazi za Wilaya na mikoa kuachana na tabia ya kuwabeba wagombea na kuchukua tahadhari kubwa na kujiepusha na kamati za fitina ambazo lengo lake ni kubomoa na sio kujenga.
Makala ametoa onyo hilo wakati wa mkutano mkuu.maalumu wa Jimbo la Kibaha mjini kwa ajili ya utekelezaji wa chama kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2020 hadi mwaka 2025 ambao umeandaliwa na mbunge Jimbo hilo SLYVESTRY KOKA.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjiini Solivestry Koka akisoma taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM 2020/2025 amesema kwamba fedha nyingi zimetolewa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ambazo zimekwenda kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo maji,afya,elimu na miundombinu ya barabara.
Nao baadhi ya wajumbe wa mkutano huo wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Mbunge wao kwa kuwaletea wananchi wake maendeleo na kutekeleza ilani kwa kishindo katika Jimbo hilo..
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.