KATIBU Mstaafu Baraza la Vijana wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mkoa wa Tanga (Bawavicha) Hemed Said amekana madai ya viongozi wa chama hicho ngazi ya wilaya wanaomtuhumu kukihujumu chama wakati wa uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika November 27, 2024.
Tuhuma hizo dhidi yake zinadaiwa ni baada ya Said kushiriki katika kikao cha pamoja na viongozi wa kisiasa wilayani Tanga ambapo Kwa pamoja walipongeza mchakato wa uchaguzi wa viongozi wa Serikali za mitaa , vijiji na vitongoji pamoja na wajumbe ambapo yeye alishiriki kama mgombea licha ya kuwa alienguliwa baada ya kukosa sifa ya kukidhi vigezo.
Akizungumza katika mkutano huo Said alisema kuna sintofahamu kwa chama hicho kumtuhumu kwamba anahusika moja kwa moja katika kuhujumu mipango ya chama jamba ambalo alilipinga kutokuhusika kutokana na kwa sasa amekwisha kustaafu na hawezi kuingia kwenye chama kwa njia yeyote bila kufuata taratibu za kichama"
" Kufuatilia kadhia hii nimekupa nikipata wasiwasi kwa sababu ninapata vitisho kwa baadhi ya wenzangu wakiwemo viongozi na wanachama changu kwamba ninahusika wakati siwezi kuhusika kwa namna yeyote ya kukihujumu chama hivyo naomba nijivue na sihusiki kwa sababu nipo ndani ya chama kwa zaidi ya miaka 15 nafahamu taratibu miongozi na kanuni zinazohusu uendeshaji wa chama" Alisema Said.
Alisema wakati alipokwenda kwenye kikao cha pamoja na viongozi wa kisiasa alikwenda kama mmoja wa wagombea ambaye alienguliwa kwa hiyo maoni aliyoyatoa ni kama mgombea aliyeenguliwa kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa .
“Sasa hapo mimi ninahusikaje na tuhuma za kuuza au kurubuni mipango au kukwamisha shughuli zozote za mafanikio ya chama changu" alihoji Said.
Aidha amesema kuwa licha ya kupokea vitisho kutoka kwa viongozi na wanachama wa chama hicho lakini hakukuwa na utaratibu wowote wa kichama ambao uliofuatwa ikiwemo kumuita kwa nia ya barua.
Kiongozi huyo Mstaafu wa Bavicha Mkoa wa Tanga amesema alishiriki kikamilifu mchakato mzima wa uchaguzi kujisaidia chama chake kusaidia kuwapatia wagombea ambao watakwenda katika uchaguzi wa Serikali za mitaa , vitongoji na vijiji.
“Tofauti zozote zinazozungumzwa kwamba Mimi nimehusika kukirubuni chama hizo sio za kweli kwa sababu nimeshiriki ndani ya chama ngazi ya wilaya kutafuta wagombea na mimi nikiwa ni mgombea wa mtaa ambao ninaoishi sasa nahusikaje kukihujuma chama “Alihoji.
“Haiwezekani nasikia wengine wanasema nimenunuliwa sio kweli nina maisha yangu ninajiendesha kila mtu anafahamu kwa sababu nina uchumi wangu binafsi" alisisitiza mwanachama huyo.
Ameeleza kuwa Chadema wilaya ya Tanga kwenye uchaguzi wa viongozi wa Serikali za mitaa vijiji na vitongoji iliweza kusimamisha wagombea 50 lakini wapo 8 ambao walijitoa wakati mchakato huo ikiendelea licha ya kukidhi vigezo alihoji kuwa wamechukuliwa hatua gani tofauti na yeye ambaye aliyeenguliwa kikanuni.
"Ndani ya chama chetu katika halmashauri ya Jiji la Tanga ambayo tuna mitaa 181 tulikuwa na wagombea 50 lakini 8 katika hao tulikuwa na mawakala 182 , je kwanini hawa 8 na Mimi na Hawa ni nani amerubunika , kama walijitoa chama kimewachukulia hatua gani mpaka mimi nionekane kama ninahusika moja kwa moja? Alihoji.
Alieleza kuwa tangu alipojiunga na chama hicho akiwa shule ya Sekondari na baadye kupata nafasi ya uongozi wa Baraza la vijana Bavicha Mkoa wa Tanga na ni miongoni mwa vijana ambao walisimama imara kukitetea chama hicho hivyo kuhusishwa na tuhuma za kukihujumu chama chake inampa wakati mgumu.
“Chama kinafahamu kuwa katika vijana ambao walisimama na kupambana kwaajili ya kukisimamisha chama Mimi ni mmoja wapo kwa sababu Nina nafasi yangu kuanzia ngazi ya chuo nimehusika kwenye project nyingi mpaka kwenye ushindi wa ubunge ambao tulipata 2015." Alisema.
Kutokana na hali hiyo amesema kwamba atawaandikia barua viongozi wa chama hicho ngazi ya wilaya kisha kupeleka nakala ngazi ya Taifa ili kidai haki yake kama mwanachama halali wa chama hicho.
Alisisitiza kuwa kila mwananchi anauhuru wa kujiunga na chama chochote na kuwa mwanasiasa ambaye anaweza kusimamia maslahi ya wananchi pamoja na Maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
"Kuchagua chama chochote cha siasa ni utashi wa mtu binafsi kwa sababu wakati ninajiunga na CHADEMA hakuna mtu ambaye alinilazimisha tupo katika harakati kwaajili ya kuwasaidia wananchi popote pale ambapo upo uweze kupaza sauti ya wananchi isikike"Alisema
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.