Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mariam Ditopile Mzuzuri akisisitiza jambo wakati wa ziara hiyo |
Na Oscar Assenga, MKINGA
KAMATI ya Kudumu ya Bunge Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo imempongeza
Rais Dkt Samia Suluhu kwa kazi kubwa anayoifanya kuchochea uwekezaji nchini
pamoja na kuweka mazingira mazuri kwa wafanyabiashara.
Pongezi hizo zilitolewa leo na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo Mariam Ditopile Mzuzuri wakati
wa ziara ya siku moja ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Uwekezaji na
Biashara ilipotembelea eneo Kituo cha Forodha za Tanzania na Kenya eneo la
Mkinga Mkoani Tanga.
Alisema kwamba mazingira hayo mazuri yamewekwa kwa
wafanyabiashara ambao tayari wapo kwenye biashara na viwanda ambavyo vinazalisha
bidhaa mbalimbal nchini
“Leo tumepata fursa ya kuja hapa kituo cha Forodha Horohoro kuona
namna kituo hicho cha pamoja baina ya Tanzania na Kenya sisi kama kamati tunawapongeza
kwani kituo hiki kazi yake kubwa kukusanya mapato kuhakikisha wafanyabishawa
kutoa Kenya wanaoleta bidhaa hawapitia njia za panya wanapitia hapo kutoa
ushuru na kodi stahiki pia bidhaa zinazotoka nchini na kwenda nchi jirani
zinatoa ushuru stahiki “Alisema
Alisema wanawapongeza kuongeza ukusanyaji wa mapato kwenye kituo
hicho kwa maana mwaka jana walipanga kukusanya jumla ya sh.Bilioni 77 lakini
walikusanya Bilioni 90 na kwa mwaka huu wa fedha wa 2024/2025 kota ya kwanza
Julai hadi Sept walipangiwa kukusanya Bilioni 25 lakini wamekusanya bilioni 34 wanaona
ni mafanikio.
“Sisi kama Kamati tunaiomba serukali na tutalisimamia lazima
waongeze ufanisi katika kituo hicho na kikubwa cha kwanza ambacho kimeelezwa ni
ununuzi wa scana kwa namna tulivyoona ukusanyaji wa mapato unaridhisha lazima
tupate scana na focklift kwa ajili ya kunyanyua mizigo tuweze kuongeza ufanisi
na mapat kupanda”Alisema
Aidha alisema kwamba inawezekana wanaotumia njia za panya ni
kutokana na kukaa muda mrefu wakati wa kupitisha mzigo na hivyo kuona shida
kupitishia hapa hivyo tunaiagiza Serikali ndani ya muda mfupi na wizara zote
husika na Waziri Dkt Jafo akae na Waziri wa Fedha ili kwa haraka scana na
focklift ziweze kupatikana na kuongeza ufanisi na kituo kifanye kazi ile
inayokusudiwa chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu na Serikali yake ya
wamu ya sita.
Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Waziri wa Viwanda na
Biashara Dkt.Suleiman Jafo amesema kwamba Serikali itahakikisha bidhaa zote
zinazopitishwa kwenye vituo vya Forodha katika mipaka ya Tanzania na nchi
jirani zinaendelea kuwa na viwango vinavyokidhi na kudhibitishwa na Shirika la
Viwango Tanzania (TBS) Wakala wa VipimoTanzania ( WMA) na Tume ya Ushindani (FCC).
Alisema kwamba lengo la kuhakikisha hilo ni kuwalinda watanzania
na walaji wa mwisho wa siku wafanye biashara na kamati imetoa maelekezo
kuhakikisha eneo hilo linakuwa na scana ambayo inaweza kuhakikisha mizigo
inakwenda kwa haraka sana.
“Hili la scana hapa tumelichukua na sio muda mrefu kupitia Wizara
ya fedha tutahakikisha Scana hiyo inapatikana pamoja nyenzo za kufanyia kazi
ikiwemo Focklift itakayokuwa ikinyanyua mizigo lakini niwashukuru Kamati ya
Bunge kwa kazi kubwa na niwaambie serikali itahakikisha mambo yote muhimu
yanatekelezwa lengo kubwa ni kuboresha utoaji huduma”Alisema Waziri Jafo.
Aidha alimshukuru R ais
Dkt Samia Suluhu kutokana na kazi kubwa inayoendelea katika maeneo mbalimbali
ya kimaendeleo na hata kamati ilivyotembelea eneo la Horohoro imeona kuna mafanikio
makubwa kwenye ongezeko la mapato.
“Lakini kuona jinsi gani Taasisi zinasaidia kuhakikisha biashara
eneo hilo mizigo isafirishwe vizuri baina ya nchi ya jirani kenya na bidhaa
zinazopita lazima zinakidhi viwango vilivyowekwa na kuthibitishwa na TBS na WMAna
FCC lengo kuwalinda watanzania na walaji mwisho”Alisema Waziri Dkt Jafo.
Akizungumzia suala la ubinafsishaji lililofanyika miaka ya nyuma
nchini alisema Serikali ilikuwa na nia njema kufanya ubinafsishaji lakini kwa
bahati mbaya malengo yalienda tofauti wengi waliopewa viwanda hawakufanya vizuri.
“Kama mnakumbuka hivi karibuni Rais Dkt Samia Suluhu alitoa
maelekezo kwamba viwanda hivyo vifufuliwe maeneo mbalimbali na nilikuja Tanga na
hivi karibuni tumekaa kikao na Hazina kubainisha viwanda vyote na kuona hatua
za kuchukua“Alisema
Waziri Dkt Jafo alisema mojawapo ya hatua hizo ni kuhakikisha viwanda
ambavyo vilikuwa havifanyi kazi waangalia namna bora ya kufanya kazi kwa
utaratibu wa kisheria na wapate wawekezaji wengine au waliokuwepo wahakikishe
ndani ya muda mfupi wanafanya uwekezaji ili viwanda viweze kufanya kazi na
kutengeneza ajira kwa watanzania.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.