NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
Jumuiya ya umoja wa wanawake (UWT) Wilaya ya Kibaha mjini imewahimiza wakinamama kuhakikisha wanajitokeza kwa wingi kuchukua fomu bila ya uwoga wowote kwa ajili ya kugombea nafasi mbali mbali za uongozi hasusan katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa ambao unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa UWT Elina Mgonja wakati wa ziara yake ya kikazi katika Kata ya tumbi na Sofu yenye lengo la kuweza kuangalia uhai wa chama pamoja na kuwahimiza wanawake kushiriki kikamilifu katika nafasi mbalimbali za uongozi.
Mwenyekiti huyo aliongeza kwamba lengo lake kubwa la kufanya ziara hiyo ni kuwatembelea wanawake katika kata zote 14 za Jimbo la Kibaha mjini ikiwa sambamba na kuangalia mwenendo mzima wa zoezi la uandikishaji wa wanachama kujisajili kwa mfumo wa kisasa kwa njia ya kieletroniki.
"Kwa kweli nimefarijika sana nimeamua kufanya ziara yangu ya kikazi ya kutembelea kata mbali mbali ambazo zipo katika Jimbo la Kibaha mjini na lengo lake kubwa ni kuweza kuangalia uhai wa chama jinsi ulivyo ikiwa sambamba na kuona namna ya zoezi zima la wanachama kujiandikisha kwa njia ya Kieletroniki,"alisema Mgonja.
Kadhalika aliwaomba wanawake wa Kata ya Tumbi pamoja na kata ya Sofu kuendelea kumpa ushirikiano wa kutosha Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan ikiwa sambaamba na kumuheshimisha katika uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kupiga kura kwa wingi ili kushinda kwa kishindo kikubwa na kuchukua mitaa yote bila kupoteza.
Kwa uapnde wake Diwani wa viti maalumu Selina Wilson amewahimiza wakinamama kutorudi nyuma katika kugombea katika nafasi mbali mbali ikiwa sambamba na kuchukua fomu kwa ajili ya kuwania nafasi mbali mbali za uongoz ikiwa sambamba na kuchangamkia fursa za mikopo zilizopo ambazo zitawasaidia katika kujikwamua kiuchumi.
Naye Diwani wa viti maalumu Shufaa Bashili amewataka wakina mama pindi wanapopata mikopo kuhakikisha kwamba wanaifanyia kazi pamoja na kuirejesha ikiwa sambamba na kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
Diwani wa viti maalumu wa Kibaha mjini Lidya Mgaya alisema kwamba wanawake wanapaswa wasiogope na kwamba wataendelea kumuunga mkono Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan katika masuala mbali mbali ya kimaendeleo.
Mwenyekiti wa UWT Wilaya yaKibaha mjini amefanya ziara yake ya kikazi katika kata mbili za Tumbi pamoja na kata ya Sofu ambapo ameambatana na baadhi ya madiwani wa viti maalumu pamoja na wajumbe wa kamati ya utekelezaji sambamba na viongozi wa chama cha mapinduzi CCM.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.