Mwanaume mmoja amefariki baada ya mfumo wa ukumbi wa michezo nyumbani aliyopokea hivi majuzi kama zawadi ya harusi kulipuka.
Kwa mujibu wa ripoti
ya polisi, bomu hilo lilikuwa limetegwa kwenye zawadi hiyo ambalo lililipuka
muda tu ilipowekwa katika umeme.
Bwana harusi huyo
ambaye alikuwa pamoja na kaka yake, alifariki papo hapo huku kaka yake
akifariki kutokana na majeraha alipokuwa akipokea matibabu.
Wakati huo huo watu
wengine wanne, akiwemo mvulana wa miezi 18, walijeruhiwa katika mlipuko huo,
ambao ulifanyika Jumatatu, Aprili 3, nyumbani kwa bwana harusi katika wilaya ya
Kabirdham katika jimbo la kati la India la Chhattisgarh
Polisi wamesema
mlipuko huo ulikuwa mkubwa kiasi kwamba kuta na paa la chumba hicho zilianguka
kutokana na athari zake.
Bomu hilo lilidaiwa
kutegwa na mpenzi wa zamani wa bibi harusi ambaye alikuwa na machungu dhidi
yake kwa kuolewa na mwanamume mwingine.
Mshukiwa kwa jina
Sarju Markam kutoka jimbo jirani la Madhya Pradesh alikamatwa Jumanne, Aprili
4.
Markam, 33, alikuwa
na uhusiano na mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 29 na alikuwa akisisitiza
kuwa awe mke wake wa pili.
Lakini familia ya
mwanamke huyo ilikataa na kupanga ndoa yake mahali pengine.
Bwana harusi amtema bibi
harusi madhabauni
Baada ya kugundua
swala la kuhuzunisha kuhusu mke wake siku ya harusi yake, bwana harusi
amefutilia mbali mipango ya ndoa.
Mwanaume huyo aligundua kwamba mrembo wake tayari alikuwa
na watoto wawili na mwanamume mwingine.
Bwana harusi huyo
ameelezea uchungu wake alipofuta mipango ya harusi na kuvua viatu vyake vya
harusi na suti.
Licha ya juhudi
kadhaa ya walioshuhudia kumtuliza, bwana harusi aliyekuwa amepandwa na mori
alikataa kuendelea na harusi.
Pia alidai
kurejeshewa mahari aliyolipa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.