Polisi nchini Indonesia wamemkamata mganga mmoja wa kijiji anayedaiwa kuwaua takriban watu 12 baada ya miili kadhaa kupatikana ikiwa imezikwa kwenye bustani ya mtu huyo.
Slamet Tohari, 45, alikiri kwa polisi kwamba makumi ya wahasiriwa
walizikwa kwenye ardhi yake.
Ameshtakiwa kwa mauaji ya kukusudia ya wateja nyumbani kwake huko
Banjarnegara katika Java ya Kati.
Polisi wamesema aliahidi kuzidisha pesa zao kwa njia za kichawi na
wateja walipotaka kurejeshewa pesa zao, aliwapa sumu.
Alikamatwa wiki moja hii baada ya mtoto wa kiume wa anayedaiwa
kuwa mwathiriwa hivi majuzi kuwaambia polisi kwamba nyumba ya Tohari palikuwa
mahali pa mwisho pa babake kwenda .
Familia ya Paryanto haikuweza kuwasiliana naye tangu machi 24
Alimweleza mwanawe eneo lake kupitia ujumbe wa WhatsApp na kumtaka
awaarifu polisi ikiwa hatarudi kufikia machi 26.
Ripoti ya polisi ilitolewa siku iliyofuata.
Polisi kisha walikwenda nyumbani kwa Tohari katika kijiji cha Desa
Balun, wilaya ya Wanayasa siku ya Jumatatu, ambapo waligundua makaburi kadhaa
ya kina kifupi katika eneo la karibu.
Baadhi ya makaburi yalikuwa na wahasiriwa wawili hadi watatu
waliozikwa pamoja.Chupa ya maji ya madini pia ilipatikana katika kila kaburi.
Polisi wanasema wahasiriwa walikuwa na umri wa kati ya miaka 25 na
50, na wengine walikuwa wamezikwa kwa miezi sita.
Miili yao haikuonyesha dalili zozote kuuawa kwa kutumia nguvu .
Haijulikani ikiwa miili hiyo imetambuliwa.Polisi hawakutoa taarifa
iwapo kumekuwa na uchunguzi kuhusu kesi hizo.
Tohari hajakanusha mauaji hayo.Hapo awali alifungwa 2019 kwa
uhalifu wa pesa ghushi na anakabiliwa na hukumu ya kifo kwa mashtaka ya sasa.
Polisi walisema alijifanya kuwa mganga, (Babu Slamet), ambaye
angeweza kuzidisha pesa utakayompatia
Waliamini kuwa Tohari amekuwa akiwaua wahasiriwa wake tangu 2020.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.