Mwanaume aitwaye Anselumu Sebuka, miaka 42, Mkulima na mkazi wa Namagondo wa kitongoji cha Kasuzu, kijiji na kata ya Namagondo, tarafa ya Mumulambo wilayani Ukerewe alikutwa ndani ya chumba chake akiwa amejaribu kujiua kwa kukata uume wake kwa kutumia kisu chenye ncha kali.
Inadaiwa Ansele Sebuka alikuwa anatuhumiwa na ndugu zake
kuiba mali mbalimbali za familia yake na za jamii inayomzunguka na kwenda
kuziuza pamoja na ulevi uliokithili ambapo waliamua kumtenga kutokana na tabia
zake.
Baada ya tuhuma hizo ndipo aliamua kujikata uume wake kwa kisu na
kuacha unaning’inia kwa lengo la kujiua.
Chanzo cha tukio hilo ni
ugonvi wa kifamilia uliopelekea mhanga kupata msongo wa mawazo.
Ansele Sebuka alipelekwa katika Hospitali ya
wilaya ya Ukerewe kwa ajili ya matibabu na hali yake inaendelea vizuri.
Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kufuata njia sahihi za
kutatua matatizo yao hususani kuwaona wataalamu wa afya ya akili ili kuepusha
madhara yanayoweza kujitokeza kutokana na msongo wa mawazo na kukosa uvumilivu
wa migogoro mbalimbali katika jamii.
Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kuacha
kujichukulia sheria mkononi badala yake watumie njia sahihi katika kuhakikisha
wanatatua matatizo yao bila kuleta madhara na usumbufu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.