ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, November 10, 2022

MAJAMBAZI WAAMURU KUPIKIWA KITOWEO CHA KUKU BAADA YA UVAMIZI


Wenyeji wa Kitengela wamelilia asasi za usalama kuwanusuru kutokana na utovu wa usalama unaoendelea kuwakosesha usingizi kila kukicha. 

Wenyeji wa eneo hilo wameripoti kwa polisi kuhusu kuvamiwa na majambazi wanaowashurutisha kuwapikia. 

 Wenyeji hao wameripoti kuwa majambazi wanaowavamia wana tabia za kiajabu, sana kwani huwalazimisha kuwapikia mlo kabla ya kuwaibia majumbani mwao. 

Mkazi wa kijiji cha Noonkopir alisimulia jinsi simu yake ilivyotwaliwa na kuamrishwa kupikaugali na kitoweo cha kuku na majambazi waliomvamia. 

Agatha Njogu aliiambia jarida la Nation.africa kuwa alipoendelea kuwapikia wavamizi hao, mmoja wao alikuwa akiwafuatilia yeye na wanao huku wengine wakizidi kuchokora nyumba na kuiba. 

 "Hawakuwa na haraka. Ni uvamizi uliopangwa kwa makini,” Njogu aliiambia the Nation. Wenyeji wamelaumu ongezeko la visa vya ujambazi, kwa utepetevu wa maafisa wa usalama eneo hilo. 

Wanadai kwamba maafisa wa kituo kidogo cha polisi cha Noonkopir, hujitokeza kwa saa chache hata ingawa wanahitajika kwa dharura. 

"Tuliamua kuweka kituo kidogo cha polisi kwa sababu ya visa vya uhalifu kwenye mtaa wetu. Ila maafisa kwenye kituo hicho huwekwa kwa saa chache kisha huondoka," mzee wa kijiji cha Noonkopir village Clement Njung'e alinukuliwa akisema.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.