Waziri wa maliasiali na utalii Balozi Dkt Pindi Chana amefungua maonyesho ya pili ya kimataifa ya karibu kusini kata viwanja vya kituo cha kikuu cha utalii kusini Kihesa Kilolo mkoani Iringa ikiwa na lengo la kutangaza vivutio vya kitalii vilivyo kusini.
Waziri wa maliasiali na utalii
Balozi Dkt Pindi Chana akiteta jambo na mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya pili ya kimataifa ya karibu
kusini kata viwanja vya kituo cha kikuu cha utalii kusini Kihesa Kilolo mkoani
Iringa ikiwa na lengo la kutangaza vivutio vya kitalii vilivyo kusini.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
WAZIRI wa maliasiali na utalii
Balozi Dkt Pindi Chana amefungua maonyesho ya pili ya kimataifa ya karibu
kusini kata viwanja vya kituo cha kikuu cha utalii kusini Kihesa Kilolo mkoani
Iringa ikiwa na lengo la kutangaza vivutio vya kitalii vilivyo kusini.
akihutubia wananchi
waliojitokeza wakati wa kufungua maeonyesho hayo, waziri wa Balozi Dkt Pindi Chana alisema kuwa imefika
zamu ya kuvitanga vivutio vya kitalii vilivyo kusini ili kuongeza watalii
kutembelea na kuongeza pato la taifa.
Balozi Dkt Chana alisema kuwa
serikali itatumia maonyesho ya kimataifa ya karibu kusini kama sehemu ya
mkakati kutekeleza ilani ya CCM ya kufikisha watalii milioni tano ifikapo mwaka
2025 na wizara ya maliasili imejipanga kimkakati ili kufikia malengo hayo na
ikiwezekana kuvuka idadi hiyo ya watalii.
alisema kuwa maonyesho hayo
yamefunguliwa rasmi yakihusisha mikoa kumi ya kusini mwa Tanzania ikiwa ni
sehemu muafaka yakutangaza utalii wa kusini.
Balozi Dkt Chana alisema kuwa
mikoa inayoshiriki maonyesho hayo ni mkoa wa
Iringa,Morogoro,Njombe,Mbeya,Songwe,Rukwa,Katavi,Ruvu Lindi na Mtwara ,mikoa
hiyo kwa kutumia maonyesho hayo itasaidia katika kutangaza vivutio vya utalii
kusini mwa Tanzania.
alisema kuwa maonyesho hayo ya
karibu kusini yenye kaulimbiu inayosema “uwekezaji,kusinifahari yetu”ni jukwaa
ambalo linawakutanisha wadau mbalimbali katika sekta ya utalii kwa lengo la
kuuza bidhaa,kutafuta masoko pamoja na kujenga mahusiano ya kibiashara kwenye
sekta mbalimbali za kitalii..
Balozi Dkt Chana alisema kuwa
kutokana na kampeni ya filamu ya Tanzania The Royal Tour ilifanywa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kumesaidia
kuongeza idadi ya watalii wa kimaoka watalii 922,692 mwaka 2019 hadi kufukia
watalii 1,034,180.
alisema kuwa mikoa ya nyanda za
juu kusini imebarikiwa kuwa na vivutio vingi vya kitalii hivy kupitia mradi wa
REGROW utasaidia kuvitangaza vivuti hivyo na kujenga kituo cha utaliiwa kusini
mwa Tanzania katika eneo la kihesa Kilolo ambacho kitatumia zaidi ya bilioni
12.
Balozi Dkt Chana alisema kuwa
serikali ya awamu ya sita imeendelea kujenga viwanja vya ndege kwa lengo la
kukuza na kuitanga sekta ya utalii ili kuongeza idadi ya watalii wa ndani na
nje ya Tanzania.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.