ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, November 7, 2022

LIVERPOOL WASEPA NA POINTI 3 MUHIMU DHIDI YA TOTTENHAM

 


Tottenham  v  Liverpool 

ALAMA 3 MUHIMU

.Jurgen Klopp aliona mapungufu ya Spurs kuacha Spaces kubwa baina ya wingbacks na mabeki wao wa pembeni kutoka ile BACK 3 yani gap baina ya Dier na Emerson na gap baina ya Davies na Sessegnon , ndio Klopp alitumia diamond shape kwenye kiungo , Bobby nyuma ya Salah na Darwin ... nini kilichotokea hasa kipindi cha kwanza ? 


.Liverpool walikuwa wanahakikisha wana hamisha mpira haraka sana kutoka upande mmoja kwenda mwingine ( switching play ) na kuvuka kiungo cha Spurs chenye viungo watatu kwa pasi za haraka .... kwa kufanya hivyo Nunez na Salah walikuwa wanapata spaces nzuri za kushambulia ndani kwasababu wingbacks wa Spurs walikuwa wanatoka kwenye nafasi zao  


.Kipindi cha pili Klopp aliona aondoke kwenye midfield diamond na kuhamia mfumo wake mama wa 4-3-3 ili kuwasaidia Robbo na TAA pembeni maana walikuwa hawana cover nzuri , bado Liverpool walikuwa wanachelewa kwenye action ya mpira ulipo hasa baada ya kuingia kwa Kulusevski ...ambaye alikuwa anazipata space mbele ya Robbo na nyuma ya Thiago . 


NOTE

1: Mo Salah yeye kazi yake kufunga haswa, mkaribishe chakula anakomba hadi mboga .. ameweka kambani magoli 9 katika mechi zake 8 zilizopita za mashindano yote : HE IS BACK 


2; Nafikiri Darwin atakuja kuwa sawa na hatari , ishara zote zipo pale kwamba ana madhara yake


3; Ukimuacha TAA 1 Vs 1 unatafuta matatizo anahitaji sana msaada 


4; MAKUBWA JINGA YA WIKI YANAJULIKANA 😀


FT : Spurs 1-2 Liverpool

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.