ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 4, 2022

BENKI YA NMB YAKUTANA NA WAFANYABIASHARA JIJINI MWANZA

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. Mhandisi Robert Gabriel amewakaribisha wawekezaji wakubwa kukamata fursa za uwekezaji zinazopatikana Mkoani humo ikiwemo ujenzi wa Hoteli za Kitalii fukwe za Ziwa Victoria na  ufugaji wa samaki wa Vizimba.

VIDEO YA TUKIO.


Ametoa wito huo mwishoni mwa wiki hii kwenye mkutano wa mtandao thabiti kwa ukuaji endelevu wa biashara, ulioandaliwa na Benki ya NMB Mkoani Mwanza na kuwakutanisha wafanyabiashara wakubwa ambapo amesema Jiji hilo lipo sehemu ya Kimkakati kutokana na kupakana na Mataifa ya jirani na kuwa kitovu cha Biashara.

 "Tuna kila sababu ya kujikita katika uchumi wa buluu, Samaki wetu wana soko zuri huko barani Ulaya hivyo tuchangamkie fursa ya Ufugaji" Mhe Gabriel


Vilevile, amesema Jiji la Mwanza bado lina nafasi kubwa ya Uwekezaji wa Hoteli za hadhi ya Kimataifa ufukweni mwa Ziwa Victoria na kusisitiza milan go ipo wazi ya ushirikiano kati ya Ofisi yake na  wale watakaokuwa tayari kwa Uwekezaji huo. 

Mkuu wa Idara ya Biashara kutoka Benki ya NMB Alex Mgeni amesema Taasisi hiyo imezidi kupiga hatua kutokana na kuweza kumkopesha mteja zaidi ya Shilingi Bilioni 200.


Katika mkutano huo na wadau, Benki hiyo imetoa mada mbambali kutoka kwa Wataalam wake kuhusu kazi za kibiashara na wateja wake na jinsi wanavyokabiliana na kuzifanyia kazi changamoto zinazojitojeza.


'Karibu mkuu........'

Kwa umakini.......






"Amani yetu ni utajiri mkubwa mno kwenye uwekezaji wa aina yoyote ile duniani, Pesa tayari tunazo, wataalamu wapo, wahandisi wapo, ni sisi tu kuona namna gani tunakuwa, tunaondoka pale tulipokaa tunaenda mahali pengine" Mhe Gabriel


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.