Tamasha hilo lilizinduliwa Juni 6,2022 na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt. Pindi Chana kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa na kufungwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Sophia Mjema Juni 7,2022.
Akizungumza wakati wa kufunga Tamasha hilo, Mhe. Mjema amewapongeza na kuwashukuru wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki tamasha la utamaduni ili kutii na kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, la kuhakikisha kila Mkoa unaenzi na kudumisha tamaduni zao hivyo kuwakumbusha wananchi kuenzi tamaduni zao kama Rais Samia anavyosisitiza mara kwa mara juu ya umuhimu wa kuenzi utamaduni zikiwemo mila na desturi.
Wananchi waliohudhuria kwenye tamasha hilo kubwa walipata fursa ya kuona filamu ya kukuza utalii nchini ijulikanayo kama The Royal Tour, iliyomshirikisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Wananchi wakiwa kwenye tamasha la Utamaduni Mkoa wa Shinyanga.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.