ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 25, 2022

CHUMI AMPONGEZA RAIS SAMIA KUPELEKA MAENDELEO JIMBO LA MAFINGA MJINI.

 

Mbunge wa jimbo la Mafinga   MjiniCosato Chumi akiongea na wananchi wa jimbo hilo wakati wa kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kupeleka maendeleo na kukuza uchumi wa wananchi wa jimbo hilo.Mbunge wa jimbo la Mafinga   MjiniCosato Chumi akiongea na wananchi wa jimbo hilo wakati wa kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kupeleka maendeleo na kukuza uchumi wa wananchi wa jimbo hilo.
Baadhi ya mabango yakionesha nini kimefanyaika jimbo la  mafinga Mjini

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kupeleka maendeleo na kukuza uchumi wa wananchi wa jimbo hilo.

 
Na Fredy Mgunda,Iringa.

Mbunge wa jimbo la Mafinga   Mjini amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kupeleka maendeleo na kukuza uchumi wa wananchi wa jimbo hilo.

 

Akizungumza wakati wa kongamano la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ambalo lilikuwa      limeandaliwa na wananchi wa jimbo la Mafinga Mjini,mbunge Cosato Chumi alisema kuwa serikali ya awamu ya sita imetoa fedha nyingi kwenye miradi ya kimaendeleo katika jimbo hilo.

 

Chumi alisema kuwa serikali ya awamu ya sita imefanikisha kuwatua ndoo akinamama baada ya kuwapelekea miradi mingi ya maji ambayo ndio itakuwa inatatua changamoto ya maji ambayo imekuwa ikiwatesa wananchi wa jimbo hilo.

 

Alisema kuwa jimbo la Mafinga limepatiwa kiasi cha shilingi bilionni 58 kwa ajili ya mradi wa maji ambao utasaidia kuongezeka kwa upatikanaji wa maji ya uhakikia kwa wananchi wote wa jimbo la mafinga

 

 "Kazi ya mbunge sio kwenda kuizodoa Serekali bungeni,Bali ni kuchukua maoni na changamoto zinazogusa maisha ya watu na kwenda kujenga hoja bungeni ili kuweza kupata ufumbuzi na mwarubaini wa changamoto za watu wako " Chumi 

 

Chumi alimpongeza waziri wa Nishati Januari Makamba kwa serikali kusitisha zoezi la uagizaji nguzo kutoka njee ya nchii,iliyozua sitofahamu na taharuki , kwani Jambo hilo lilikuwa linaenda kuuwa uchumi wa watu wengi.

 

Alisema kuwa maamuzi ya serikali yamekuwa na manufaa kwa wananchi wa mikoa ya Iringa,Njombe na Tanga ambako ndio haswa wanazalisha nguzo za umeme na kuongeza ajira kwa wananchi ambao wapo kwenye sekta ya misitu.

 

Chumi alimpengeza rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya kuleta maendeleo kwa taifa na wilaya ya Mufindi hasa pale alipoamua kutenga bajeti ya ujenzi kwa kiwango cha lami kwa Barabara ya Mafinga ,mgololo,Nyololo ambayo sasa itachochea kukua kwa uchumi kwa wananchi wa wilaya hiyo.

 

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi Daud yassin alisema kuwa anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa madarasa katika shule zote za wilaya hiyo.

 

Yassin alisema kuwa fedha za UVIKO 19 zilisaidia katika ujenzi wa madarasa na kuwapunguzia michango kwa wananchi wote wa watanzania.

 

Alisema kuwa wilaya ya Mufindi imenufaika na fedha kwenye miradi ya elimu na afya ambayo hapo awali ilikuwa ngumu sana kupata fedha hizo kwenye miradi mbalimbali.

 

Yassin alisema kuwa katika bunge la bajeti la mwaka wa 2022/2023 wamepewa ujenzi wa barabara ya Mafinga mgororo ambayo ilikuwa kilio kwa wananchi wa wilaya ya Mufindi kwa ajili ya kukuza uchumi.

 

Alisema kuwa kwa kiasi kikubwa uchumi wa wananchi wa Mufindi unategemea barabara hiyo ambayo imekuwa ikipitisha bidhaa mbalimbali za mazao ya misitu ambayo ndio kitovu cha uchumi kwa wanamufindi wote.

 

 Yassin alimazia kwa kusema kuwa chama cha mapinduzi CCM wilaya ya Mufindi wanafanya kazi kwa ushirikiano mzuri na serikali ya wilaya ndio maana kimekuwa na mafanikio makubwa ya kimaendeleo na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo.


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.