Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro akizindua ofisi mpya ya kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Iringa iliyojengwa kwa zaidi ya Sh Milioni 100 kwa msaada wa kampuni ya Ivori Iringa.
Na
Fredy Mgunda,Iringa.
MKUU wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro amezindua ofisi mpya ya kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Iringa katika kituo kikuu cha Polisi cha mjini.
Wakati ofisi ya kikosi cha usalama barabarani imejengwa kwa msaada wa kampuni ya Ivori Iringa ambayo inazalisha bidhaa za Ivori.
Akizindua jingo hilo IGP Sirro alimshukuru mkurugenzi wa kampuni yaIvori kwa michango wake mkubwa akisema inasaidia kuliongezea jeshi hilo ufanisi katika utendaji wake kazi.
“Nawashukuru Ivori Iringa kwa misaada yao kwa jeshi la Polisi. Wafanyabiashara wengine acheni ubahiri, kama hakuna ulinzi, hamuwezi kulala kwa raha kwani mtakuwa na hofu kubwa ya kuibiwa mali zenu. Nawaomba mjitokeze kulichangia jeshi la Polisi ili lifanye kazi yake sawasawa,” alisema.
Alisema Jeshi la Polisi ni mali ya wananchi na kwa muktadha huo wanatakiwa kulipa ushirikiano ukiwemo wa kusaidia kuboresha mazingira ya utendaji wake kazi.
Alizungumzia pia ulinzi shirikishi akisema Jeshi la Polisi haliwezi kuifanya kazi ya kulinda wananchi na mali zao pekee yake.
“Halmashauri zitunge sheria za ulinzi shirikishi ili katika maeneo yote kuwepo na vikundi vya kijamii vinavyofanya ulinzi mitaani kwa gharama za wananchi wenyewe, " alisema na kuwataka hata wale wananchi wenye walinzi wao binafsi au silaha kuchangia ulinzi shirikishi maarufu kama polisi jamii.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Ivori Iringa, Suhail Esmail Thakore alisema waliamua kujenga jengo hilo la usalama barabarani kwa kuwa wanatambua kazi kubwa inayofanywa na kikosi hicho na jeshi la Polisi kwa ujumla wake katika kulinda wananchi na mali zao.
Takore alisema wameamua kujenga jengo hilo la usalama barabarani kwa kuwa wanatambua kazi kubwa inayofanywa na jeshi la polisi kwa ujumla.
“Tutaendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kadri tutakavyopata fursa. Sisi ni wadau na tunaamini tunatakiwa kuwa sehemu ya usalama wa Taifa hili,”alisema.
Thakore alisema wataendelea kushirikiana na jeshi la Polisi katika nyanja mbalimbali ili kurahisisha utendaji kazi wake.
Aliwataka wananchi kushirikiana na jeshi hilo kukabiliana na makosa ya usalama barabarani, na uharifu vikiwemo vitendo vya ukatili wa kijinsia na ubakaji wa watoto.
Naye Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, ACP Allan Bukumbi alimueleza IGP Sirro kwamba vitendo vya uharifu mkoani Iringa vimeendelea kupungua kupitia mikakati mikubwa waliyonayo ya kukabiliana na vitendo hivyo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.