ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, June 13, 2022

CCTV YANASA MAJAMBAZI 6 WAKIMVAMIA MWANADADA WAKIWA NA BUNDUKI NA MAPANGA

 CCTV Yawanasa Majambazi 6 Wakimhangaisha Mwanadada Ndani ya eneo la uwa wa nyumba yake hadi ndani ya Jumatatu.

Kanda ya video iliyonaswa na kamera ya CCTV imeibuka kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha mwanamke akishambuliwa na majambazi waliokuwa wamejihami na kujifunika nyuso zao ndani ya ua wa nyumba yeke huko Gataka, Rongai. Katika video hiyo ambayo Jembe fm nayo imeitizama, mwanamke huyo alikabiliwa na majambazi sita mara baada ya kuingia ndani ya boma lake kwani lango lake lilikuwa bado liko wazi. Kama inavyoonekana kwenye video hiyo ambayo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii, wahalifu wawili walikuwa na bastola, mwingine alikuwa na panga na bunduki ya AK47. Katika tukio hilo lililoripotiwa kutokea usiku wa Jumapili, Juni 12, majambazi hao walionekana kumtaka mwanamke huyo ashuke kwenye gari lakini alikaidi. Alijaribu kutoa gari bila mafanikio. Majambazi hao walitumia panga kuvunja vioo vya gari lake. Mmoja wa majambazi hao, aliyekuwa amevalia balaclava, alitumia zaidi bastola yake kuvunja dirisha la upande wa dereva. Baada ya kufanikiwa kuuvunja mlango na kuufungua, majambazi hao walimkokota binti huyo kutoka nje ya gari. Kisha, waliipora na kuchukua vitu vichache, vinavyoonekana kuwa pesa. Kisha wangemvuta mwanamke huyo hadi nyumbani kwake. Muda wote huo walimnyooshea bunduki huku akiwaomba wasimuumize. Akiwa ndani ya nyumba hiyo, picha za CCTV zilionyesha majambazi hao wamhangaisha. Wakamsukuma hadi kwenye kochi. Kisha wakamwomba avue viatu vyake vya mchuchumio na kumuingiza kwenye chumba kingine. Majambazi wengine wanaonekana wakiokota baadhi ya vitu vya thamani na kuvificha kwenye begi. Baadhi ya vitu walivyochukua kutoka nyumbani ni pamoja na simu na vifaa vingine vya kusikizia muziki.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.