ZAIDI ya vijana 100 mkoani Mwanza, wameunda umoja wa mabalozi wa Sensa wa kujitolea kwaajili ya kusaidia tukio la Sensa lipate matokeo chanya.
Wakitangaza mikakati yao jijini Mwanza Mei 17, 2022 Mwenyekiti wa umoja huo Mansour Jumanne amesema wameguswa na umuhimu wa Sensa, kwani ina faida kubwa kwa maendeleo ya Taifa. Mwenyekiti huyo aliitaka jamii ihamasike na kutoa ushirikiano mkubwa kwa suala la Sensa ili taifa liweze kupata takwimu ya idadi ya watu na kupanga mipango ya maendeleo. Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Cahama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Nyamagana, Boniphace, amesema wamehamasika kwaajili ya umuhimu wake kwa taifa, akisema wanataka kusaidia kusukuma mbele juhudi za serikali kufanikisha kazi hiyo. Umoja huo unaundwa na kada ya vijana tofauti wakiwemo waandishi wa habari, wanafunzi wa vyuo vikuu, wasanii, wanasheria, wakulima, wafanyabiiashara wadogo (machinga), wavuvi, waganga na wauguzi.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.