MAADHIMISHO ya Siku ya Kutokomeza Fistula Duniani, Kitaifa nchini Tanzania yatafanyika jijini Mwanza katika viwanja vya Hospitali ya Rufaa ya Bugando.
Maadhimisho hayo yanafanyika wakati Mikoa ya Kanda ya Ziwa ikitajwa kuongoza kwa idadi kubwa ya akinamama wenye changamoto hiyo. Jembe Fm imepata nafasi ya kuzungumza na Dr. Elieza Chibwe ambaye ni Daktari Bigwa wa Magonjwa ya Afya, Uzazi, pia ni Mratibu wa Huduma za Fistula toka Hospitali ya Rufaa ya Bugando ya jijini Mwanza, hapa akitanabaisha kuwa matibabu ya Fistula yanatolewa BURE kutoka hospitali hiyo. Tarehe 23 Mei ya kila mwaka, Tanzania huungana na nchi nyingine Duniani kuadhimisha siku ya kimataifa ya kutokomeza Fistula ya uzazi. Huu ni Mwakani wa tisa tangu tulipoanza kuungana na mataifa mengine Duniani kuadhimisha siku hii. Kauli mbiu ya maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Fistula kwa mwaka 2022 ni: “Tokemeza Fistula, Wekeza, Imarisha Ubora wa Huduma za Afya na Wezesha Jamii” (End Fistula, Invest in Quality Health Care, Empower Communities) Ujumbe huu unaelekeza kila mtu na serikali kuhakikisha ugonjwa wa Fistula unatokomezwa na wanawake wanaopata matatizo haya hawatakiwi kunyanyasika kwenye jamii zao na wana haki za kupata huduma bora. Serikali kupitia Wizara ya Afya ikishirikiana na wadau wa maendeleo wanatakiwa kuwekeza zaidi kwenye huduma bora za Fistula nchini. Aidha, ujumbe unasisitiza wahudumu wa afya kuzingatia utoaji wa huduma bora za Fistula kwa kuzingatia usawa. Hivyo basi, ni wajibu wetu kuangalia tulipotoka, tulipo na kufikiri namna gani tutalimaliza tatizo la Fistula Tanzania.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.