ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, April 10, 2022

MMOJA AFA AJALI YA BASI LIKIGONGA LORI PWANI.

 


Mtu mmoja amefariki dunia papohapo na wengine wawili kujeruhiwa baada ya basi la abiria kugonga lori katika eneo la Mdaula mkoani Pwani.


Ajali hiyo ambayo imehusisha basi la Radis Samwel liliokuwa linatoka Kahama kwenda Dar es Salaam ambalo limegonga lori kwa nyuma imetokea usiku wa kuamkia leo Jumapili Aprili 10, 2022.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani (RPC), Pius Lutumo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa imesababisha kifo cha mtu mmoja na majeruhi wawili.


“Ni kweli taarifa hizo, inasemekana amefariki mtu mmoja kwenye ajali hiyo ambayo imehusisha basi na lori, basi lilikuwa linatoka Kahame kwenda Dar es Salaam lakini bado naendelea kufuatilia” amesema


Amesema kuwa ajali hiyo imetokea baada ya basi lililokuwa likijaribu kulipita lori lililokuwa mbela na kuligonga.


Kamanda Lutumo amesema bado anaendelea kufuatilia taarifa za ajali hiyo huku akaahidi kutolea taarifa zaidi baadaye.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.