Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Upandaji Miti Kitaifa na Siku ya Misitu Duniani mwaka 2022 yatakayofanyika Wilayani Magu, mkoani Mwanza yakiongozwa na Kaulimbiu isemayo 'MTI WANGU, TAIFA LANGU, MAZINGIRA YANGU, KAZI IENDELEE'.
Maadhimisho hayo yatafanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania yakiwa yameongozwa na malengo makuu mawili ambayo ni kuwakumbusha na kuwahamasisha Watanzania kuhusu umuhimu wa upandaji na utunzaji wa miti kwa ajili ya kuongeza upatikanaji wa bidhaa na huduma za misitu hapa nchini.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.