ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, March 21, 2022

MTOTO WA MIAKA 14 MBARONI KULAWITI WENZIE 19

 


Jeshi la Polisi mkoani Iringa linamshikilia mtoto mwenye umri wa miaka 14 kwa tuhuma za kuwalawiti watoto wenzake 19.


 Mtoto huyo anadaiwa kutumia pipi na biskuti kama njia ya kuwalaghai wenzake ili akamilishe adhma yake ya kuwalawiti.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi amesema mtoto huyo amekamatwa baada ya ofisa Mtendaji wa Kata ya Kihesa Kilolo, Elizabeth Lugenge kutoa taarifa ya kuwepo kwa watoto watatu wanaosoma katika shule ya Msingi Igeleke kulawitiwa.


Amesema baada ya mahojiano, watoto hao walikubali na kuwataja wenzao watano.


“Na hao watano walipohojiwa wakawataja wengine watano hivyo kufanya idadi ya watoto 13. Mtuhumiwa alipohojiwa alikubali na akawatraja watoto wengine sita, wakawa 19,” amesema Bukumbi.


Amesema mtuhumiwa amesema alikuwa akichukuwa fedha kwa bibi yake, ananunua pipi kama mbinu ya kuwapata wenzake ili awafanyie kitendo hicho.


“Kwa hiyo watoto walipokuwa wanaenda kuangalia TV aliwagawia pipi na biskuti kama njia ya kuwalaghai,” amesema.


Ameeleza kuwa watoto wote waliotajwa walipelekwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa na Frelimo na uchunguzi ukabaini kuwa wamelawitiwa.


“Kesi nane zimefunguliwa na upelelezi umeshakamilika hivyo atapelekwa mahakamani, watoto hawa walikuwa wakifanyiwa hivyo kwa nyakati tofauti,” amesema.


Mbunge wa Jimbo la Iringa, Jesca Msambatavangu amesema ubakaji na ulawiti umekuwa tishio katika Manispaa ya Iringa jambo linalohitaji nguvu ya ziada kupambana nalo.


“Fikiria hili tukio sio la mara moja, hawa watoto walikuwa wakifanyiwa mara kwa mara lakini wazazi hawakujua, ila mtendaji wa kata alipata taarifa shuleni. Tunakwama wapi wazazi na wale? Hili ni tatizo,” amesema Bukumbi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.