ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, August 18, 2021

MWANDISHI WA MILLARDAYO.COM MWANZA AFARIKI DUNIA KWA AJALI.

Enzi za uhai wake marehemu Nelson Brigeri ‘Nelly TZA.
 ⚫▶Nimeumizwa na taarifa za msiba wako mdogo wangu Nelly umekuwa mpiga picha mahiri na fundi wa MillardAyo.Com Mwanza, ...............Amefariki dunia kupitia ajali mbaya eneo la Kibaha usiku wa kuamkia leo baada ya kugongana uso kwa uso na gari ya mizigo.

.

Walikuwa watatu kwenye gari private ambapo wengine waliokuwa naye ni pamoja na Dullah TZA (yuko hospitali akipatiwa matibabu) na mfanyabiashara wa magari wa jijini Mwanza Mujitaba Yusuf Abbas (PICHANI CHINI).

Enzi za uhai wake marehemu Mujitaba Yusufu Abbas

"Binafsi moyo wangu umekunjika, unauma, hofu imenitanda, huruma kwa rafiki ambaye alikuwa mpole na mtiifu, .......oh my....." 😭😭😭

Taarifa zinaeleza kuwa ndani ya gari hilo dogo binafsi kulikua na watu watatu ambapo mmoja wao, Nelly amepoteza maisha pamoja na Mujitaba naye amefariki dunia.
 Dullah (pichani) aliyepata majeraha anaendelea na matibabu.Uongozi na Wafanyakazi wa Jembe Fm pamoja na Gsengo Blog tunatoa pole kwa Mkurugenzi wa Ayo TV, Millard Ayo, wafanyakazi wote wa Ayo TV, ndugu pamoja na marafiki kwa kuondokewa na mpendwa wao.

Mwenyezi Mungu azilaze mahali pema peponi za marehemu, AMEN!

#RiPElly

#RiPMujitaba 

CC:- #KaziNaNgoma

@bongewajue

@mustafakinkulah 

@kikotifredy 

@florenciapeter_tz


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.