ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, March 13, 2020

OCODE YAMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI KWA KUWAJENGEA DARASA JIPYA WANAFUNZI WA KIBWEGERE

 Mkurugenzi wa shirika la Ocode Joseph Jackson wa kati kati akiwa na Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya ubungo Beatrice Dominic  wa kushoto pamona na Afisa elimu wa manispaa hiyo  kulia wakiwa wameshikilia upete kwa ajili ya kuukata ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa darasa moja la wanafunzi wa elimu ya awali Kibwegere ambalo limetolewa na shirika la  Ocode kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
 Baadhi ya wanafunzi wanaosoma katika shule ya msingi Kibwegere elimu ya awali wakiwa wameketi katika madawati ambayo yametolewa kwa msaada wa shirika la Ocode katika halfa ya makabidhiano yaliyofanyika katika viwanja vya shule hiyo manispaa ya ubungo Jijini Dar es Salaam/(PICHA NA VICTOR MASANGU)
 Mkurugenzi wa Shirika la Ocode Joseph Jackson akizungumza na baadi ya walimu, wanafunzi wa shule ya msingi Kibwegere hawapo pichani wakati wa halfa ya makabidhiano ya uzinduzi wa darasa jipya ambalo limejengwa kwa ajili ya wanafunzi wa elimu ya awali kwa ajili ya kuwasaidia waweze kusoma katika mazingira ambayo ni rafiki.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
 Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic akifafanua jambo kwa walimu na wanafunzi ambao walihudhulia katika halfa fupi ya makabidhiano ya chumba cha darasa jipya ambacho kimejengwa kwa ajili ya kusomea watoto wa elimu ya awali.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
 Mkuu wa Shule ya Msingi Kibwegere Charles Kulemba akisoma Risala mbele ya mgeni rasmi wakati wa halfa ya uzinduzi huo wa darasa jipya mablo limejengwa mahusus kwa ajili ya watoto wadogo wanaossoma katika ngazi ya awali.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
 Mmoja wa walimu ambao wanawafundisha wanafunzi wa elimu ya awali Bi. Eunice Matembo akisoma Risala yake kwa mgeni rasmi amabye ni  Mkurugenzi mteandaji wa Manispaa ya Ubungo hayupo picha wakati wa halfa hiyo ya makabidhiano ya madawati, viti pamoja na uzinduzi rasmi wa darasa hilo la wanafunzi wa awali.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
 Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic wa katikati akijadiliana  jambo na mwalimu mkuu wa Shule hiyo ya Kibwegere pamoja na watumishi wengine wa Ocode na serikali wakati wa halfa hiyo ya makabidhiano wa misaada mbali mbali ikiwemo meza pamoja na viti kwa ajili ya kukalia walimu.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
 Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Kibwegere wakiwa wanasikiliza hotuba ambayo ilikuwa inatolewa na Mkurugenzi wa shirika la Ocode Joseph Jackson hayupo pichani wakati wa sherehe ya uzinduzi wa darasa  jipya ambalo limejengwa kwa ajili ajili ya kuwasaidia watoto wa elimu ya awali.(PICHA NA VICTOR MASANGU)
 Baadhi ya watendaji wa Shirika la Ocode wakiwa wameketi kwa utulivu wakifuatilia hotuba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic hayupo pichani wakati wa halfa hiyo ya uzinduzi wa darasa moja jipya lililojengwa kwa ajili ya wanafunzi wa elimu ya awali.(PICHA NA VICTOR MASANGU)

Pichani ni kibao ambacho kinaonyesha shule ya msingi Kibwegere iliyopo katika Manispaa ya Ubungo iliyopo Jijini Dar es Salaam.abpo shule hiyo imepatiwa msaada wa madawati, 39 viti 13 vya walimu pamoja na kukabidhiwa darasa jipya kwa ajili ya watoto wa elimu ya awali lililotolewa na shirika la Ocode na kughalimu kiasi cha shilingi milioni 24 (PICHA NA VICTOR MASANGU)
NA VICTOR MASANGU, UBUNGO
SEKTA ya elimu hapa nchini licha ya serikali ya awamu ya tano kuweka  sera ya kutoa elimu bure lakini bado katika baadhi ya maeneo ya shule za msingi na Sekondari zilizopo katika Manispaa ya Ubungo Jijini Dar es Salaam zinakabiliwa na changamoto mbali mbali ya upungufu wa matundu ya vyoo pamoja  na uhaba na uchakavu wa  miundombinu ya madarasa hivyo kusababisha wanafunzi wengine kusoma katika mlundikano mkubwa.
Katika kuliona hilo Shirika lisilokuwa la kiserikali la Organization Community Development (OCODE)  limeamua kumuunga mkono Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli katika kuboresha sekta ya elimu kwa kutoa msaada wa madawati 39,ya wanafunzi, viti 13 vya kukalia walimu pamoja na kukabidhi rasmi chumba cha darasa moja jipya  kwa ajili ya wanafunzi wa elimu ya awali katika shule ya msingi Kibwegere.
Akizungumzia kuhusiana na msaada huo Mkurugenzi wa Shirika la Ocode Joseph Jackson amesema kwamba kwa sasa wana tekeleza mradi wa elimu ambao utakuwa wa  kipindi cha miaka mitano ambao umeanza kufanyika tangu 2019- 2023 kwa lengo la kuwez kuwasaidia watoto wa shule za awali na msingi katika kuwawekea mazingira mazuri katika suala zima la upatikanaji wa kupata elimu iliyo bora kwa manufaa yao ya baadae.
 Aidha Mkurugenzi huyo alibainisha kwamba katika mradi huo umeweza kugusa ujenzi wa darasa hilo jipya la wanafunzi wa elimu ya awali ambalo mpaka kukamilika kwake limegharimu kiasi cha shilingi milioni 26 na kwamba wana imani kuwa watoto hao kwa sasa waliokuwa wanakabiliwa na changamoto ya kukaa kwa mlindikano watasoma katika mazingira ambayo ni rafiki kwao

“Shirika letu la Ocode kwa sasa linaendelendea kutekeleza program ya mradi wa elimu ambao utakuwa unazigusa baadhi ya shule za msingi ambazo zipo katika maeneo mbali mbali ya Jiji la Dar es salaam, maana nia yetu ni kuwasaidia watoto hawa kuanzia elimu ya awali na kwamba kwa sasa tutajikita zaidi kwa wanafunzi wa daras ala kwanza na darasa la pili pamoja na wale wanafunzi wa ngazi ya awali ili kuweza kuwajengea uwezo wa kupata elimu bora,”alisema Mkurugenzi huyo.
Pia alibainisha kwamba katika kipindi cha utekelezaji wa mradi huo kwa kipindi cha miaka mitano watahakikishwa kwamba wanashirikiaa bega kwa began a serikali ya awamu ya tano pamoja na wadau wengine wa maendeleo ili kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo kupitia elimu kuanzia ngazi za chini na kuendelea.
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Kibwegre  akisoma risala kwa mgeni rasmi katika halfa ya makabidhdiano ya madawati na  uzinduzi wa  darasa hilo amebainisha kwamba kwa sasa wanafanya kazi katika mazingira magumu sana kutokna na ukosefu wa ofisi za walimu na vyumba vya madarasa ambapo wakati mwingine inawalazimu walimu kufanyia kazi zao wakiwa wamekaa chini ya miti hivyo msaada huo ambao umetolewa na Ocode utakuwa ni mkombozi kwa upande wao.
“Shule yetu ya Kibwegere kwa kweli tunapenda kutoa shukrani zetu za kipekee kwa Shirika ili la Ocode kwani wameweza kutuona na kutusaidia katika mambo mbali mbali  ya kutujengea darasa moja, kutupa viti, pamoja na madawati ya wanafunzi hii kwa upande wetu ni moja ya hatua, kwani hapo awali hali ilikuwa ni ngumu kutokana na miundombinu yenyewe ya madarasa pamoja na ofisi za walimu, hivyo napenda kushukuru sana,”alisema Kulemba.
Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Manispaa ya Ubungo Beatrice Dominic ambaye alikuwa mgeni rasmi katika halfa ya makabidhiano amesema kwamba pamoja na juhuzi zinazofanywa na serikali lakini amekiri bado kunachanagmoto kubwa ya miundombinu ya madarasa kwa shule ya msingi na sekondari na anatambua walimu wanafanya kazi zao katika mazingira magumu sana hivyo amelipongeza shirika la Ocode kwa kuamua kushirikiana na serikali katika kuboresha sekta ya elimu kuanzia ngazi ya awali.
SHULE ya msingi Kibwegere iliyopo katika Manispaa ya Ubungo nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam  kwa sasa ina jumla ya wanafunzi 1741 ambao wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo upungufu wa walimu, uhaba wa miundombinu ya madarasa, ofisi za walimu, pamoja na matundu ya vyoo.
                                                          MWISHO .

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.