ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, February 11, 2020

ALIYECHANA QURAN TUKUFU AFUKUZWE KAZI MOJA KWA MOJA.

Rais  wa muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli  amemuagiza waziri  Suleimani Jafo kumfukuza kazi moja kwa moja mtumishi aliyechana Quran tukufu kilosa mkoani Morogoro.

Kauli hiyo ameitoa leo akiwa,Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es Salaam wakati akizindua jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni na Jengo la Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni.


“Juzi nilkuwa namsikiliza Waziri Jafo yupo Mtumishi alichana Quran nafurahi umemsimamisha kazi, lakini naagiza afukuzwe moja kwa moja, ashinde kesi asishinde ila aondoke, muandikie barua ya kumfukuza, akitoka huko atajua mwenyewe atakakoyatafuta Maisha”- JPM


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 11, Febuari, 2020 anazindua Jengo la Manispaa ya Kigamboni na Jengo la Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni katika Eneo la Gezaulole Kigamboni Jijini Dsm.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.