VIDEO.
Shirika la kutetea haki za wanawake na
watoto KIVULINI limekabidhi vyeti na kompyuta mpakato 11 zenye thamani ya
shilingi milioni 13.2 (Tsh. 13,200,000) kwa viongozi mbalimbali wanaoshiriki
vema kwenye mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto
katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela pamoja na Halmashauri ya Wilaya
Misungwi.
Akizungumza jana Julai 12, 2019 kwenye
zoezi la kukabidhi zawadi hizo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI,
Yassin Ally alisema hatua ni sehemu ya kutambua utendaji kazi bora wa viongozi
hao ambao wamesaidia utekelezaji kampeni ya kutokomeza ukatili wa kijinsia
ikiwemo mimba na ndoa za utotoni kwa wanafunzi.
Aidha Yassin alibainisha kwamba kupitia
juhudi za viongozi hao, kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi pia kimeongezeka
katika matokeo ya kidato cha sita mwaka huu 2019 katika shule mbili za mfano
ambazo ni Shule ya Wasichana Bwiru pamoja na Misungwi Sekondari.
Sanjari na kuainisha kuwa Serikali bado itaendelea kuwadhibu vikali bila kuangalia sura wanaume watakao kutwa na hatia ya kuwapa mimba wanafunzi, Mbunge wa jimbo la Ilemela ambaye
pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline
Mabula aliyekuwa mgeni rasmi, ametoa rai kwa shirika la KIVULINI kuendelea kusaidia
utoaji elimu hadi ngazi ya jamii ili kusaidia kuimarisha mapambano dhidi ya ukatili wa
kijinsia, ambao pia unamadhara kwa afya ya akili ya mtoto wa kike.
Viongozi waliopata vyeti na kompyuta
mpakato (Laptops) ni mbunge jimbo la Ilemela, Mstahiki Meya Manispaa ya
Ilemela, Mkurugenzi Manispaa ya Ilemela, Afisa Elimu Sekondari Ilemela, Mkuu wa
Shule ya Wasichana Bwiru.
Wengine ni Mkuu wa Wilaya Misungwi,
Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya Misungwi, Afisa Elimu Sekondari Misungwi, Afisa
Maendeleo ya Jamii Misungwi, Mkuu wa Shule ya Sekondari Misungwi pamoja na
aliyekuwa Mkurugenzi Halmashauri ya Misungwi ambaye amehamishiwa Halmashauri ya
Chato.
Mbunge wa jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula akizungumza baada ya zoezi la kukabidhi kompyuta mpakazo kwa viongozi mbalimbali Ilemela na Misungwi.
Mbunge wa jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula (kushoto) akikabidhi cheti kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela, Renatus Mulunga (kulia).
Mbunge wa jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula (kushoto) akikabidhi kompyuta mpakato (laptop) kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela, Renatus Mulunga (kulia).
Mbunge wa jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula (kulia) akikabidhi kompyuta mpakato (laptop) kwa Afisa Elimu Sekondari wilayani Misungwi, Mwl. Diana Kuboja (kushoto).
Mbunge wa jimbo la Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula (kulia) akikabidhi kompyuta mpakato (laptop) Afisa Maendeleo ya Jamii wilayani Misungwi.
Jedwali likionesha kiwango cha ufaulu kilivyopanda katika Shule ya Wasichana Bwiru wilayani Ilemela pamoja na Misungwi Sekondari wilayani Misungwi kuanzia mwaka 2016 hadi mwaka huu 2019.
Wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto.
Viongozi mbalimbali wakiwemo Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.