ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, July 21, 2019

SIMU YA MAGUFULI YANASUA MAKONTENA YALIYOKWAMA BANDARINI HATIMAYE YAWASILI MWANZA


Rais Magufuli akimpigia simu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Doto james siku ya Jumanne Julai 16, 2019.

Baada ya Rais Magufuli kukagua ujenzi wa Cherezo pamoja na ukarabari wa Meli jijini Mwanza siku ya Jumanne Julai 16, 2019 na kubaini baadhi ya makontena yenye vifaa yamekwama bandarini hatimaye yameanza kufika Mwanza.

Akiwa jijini Mwanza JANA Julai 20, 2019, Naibu waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Elias Kwandikwa amepokea makontena 10 ya vifaa vya ujenzi huo wa cherezo pamoja na ukarabati wa meli za MV Butiama na MV Victoria.

Malori yaliyobeba Makontena yakiwasili Mwanza.
Baada ya kubaini makotena hayo yamekwama Mwanza, Rais Magufuli alimpigia simu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James na kumtaka ahakikishe taratibu zote zinakamilika kwaajili ya makontena hayo kufika Mwanza kwa wakati.
Aidha makontena 10 yaliyofika Mwanza na kupokelewa na Naibu Waziri Kwandikwa ni sehemu ya makontena 56, ambayo awali yalikuwa yamekwama Dar es Salaam.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.