Miss Morogoro 2019 Shubila Staton akipungia mkono wageni waalikwa walifika katika shindano la kumsaka mlimbwende wa mjini kasoro bahari Morogoro mara baada ya kutangazwa.
Miss Morogoro 2019 Shubila Staton atoa machozi ya furaha baada ya kutangazwa kubeba taji hilo. Pembeni yake kulia ni Meya wa Manispaa ya Morogoro Paschal Kihanga, Miss Morogoro namba mbili Moureen Kaaya na kulia ni muandaaji wa mashindano hayo Farida Fujo.
Wadhamini wa shindano hili, DSTV wakitoa zawadi kwa washindi wa tatu wa Miss Morogoro 2019.
Muandaaji wa Miss Morogoro 2019 Farida Fujo akitoa neno la nasaha kwa washiriki na shukrani kwa wageni waliofika katika shindano hilo lililofanyika mjini Morogoro July 20, 2019.
Muandaaji wa Miss Morogoro 2019 Farida Fujo (katikati) akiwa na Msimamizi wa Mshindano hayo Martini Kadinda (kulia) na kushoto ni Msanii wa bongo movie Irene Uwoya.
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG, Morogoro.
Mbio za kumtafuta Miss Morogoro 2019 zimefikia tamati alfajili ya leo ambapo mrembo Shubila Staton ameibuka kidedea kwa kuwaangusha warembo wenzake 12 na kupata nafasi ya kuwakilisha mkoa wa Morogoro katika mashindano ya Miss Tanzania.
Akimtangaza mshindi huyo msimamizi wa mashindano hayo Mbunifu wa Mavazi Martin Kadinda alianza kwa kutangaza walioingia sita bora na baade tatu kumalizia mshindi.
Katika shindano hilo warembo hao walipanda jukwaani na kuonyesha mavazi ya aina mbalimbali ikiwemo vazi la Ubunifu, vazi la jioni, navazi la ufukweni ambapo mlimbende Shubila Staton kushika nafasi ya kwanza huku nafasi ya pili ikichukuliwa na Moureen Kaaya na nafasi ya tatu ameshinda Veronica Royal.
Akitoa neno mgeni rasmi Meya wa Manispaa ya Morogoro Paschal Kihanga amewashukuru waandaaji wa shindano hilo kwa kulifanya la wazi na haki na linaloletea heshima katika mkoa.
"Binafsi nimefurahishwa na waandaaji kwa kuendelea kuuletea heshima mkoa wetu kwa mwaka wa pili mfululizo," amesema.
Kwa upande wake muandaaji wa Miss Morogoro 2019 Farida Fujo amewashukuru wakazi wa Morogoro kwa kuendelea kuwaamini kwa miaka miwili mfululizo jambo linalowapa heshima ya pekee.
Mashindano yaliyoandaliwa na Nyumbani Park ambao ni wamiliki wa kiwanja cha burudani cha Samaki Spot kilichopo mjini Morogoro yalikuwa na ushindani mkubwa kwa vile yalikuwa na warembo wenye viwango.
Ni usiku ulipambwa na burudani za aina yake kutoka kwa wasanii Barnaba, Christian Bella na watu mashughuli nchini akiwemo Irene Uwoya, mama Dangote, Ndama mtoto wa ng'ombe, msanii Steve Nyerere huku shauku kubwa ya mashabiki wa sekta ya urembo mkoani Morogoro ni kushudia nani anatwaa taji la miss Morogoro mwaka 2019 kati ya walimbwende 12 walioshiriki shindano hilo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.