ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 15, 2019

KOMBORA LAANGUKA KARIBU NA UBALOZI WA MAREKANI.


Kombora limeanguka katika nyumba moja karibu  na ubalozi wa Marekani katika mji wa mkuu wa Baghdad nchini Iraq.

Kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa kutoka kitengo ya Mawasiliano ya Usalama wa Wizara ya Ulinzi ya Iraq, kombora la aina ya Katyusha limeanguka ndani ya nyumba katika eneo la al-Cadiriya katikati mwa Baghdad.

Hata hivyo kombora hilo halikusababisha uharibifu wowote.

Taarifa zaidi kuhusu kombora hilo haijatolewa.

Kwa upande mwingine, kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kutoka chanzo cha usalama, kombora hilo limeangukia nyumba inayoangaliana na Ubalozi wa Marekani mjini Baghdad.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.