ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, April 1, 2019

HUSSEN PENDEZA NA JUMA RAMADHANI 'CHOKI' KUZIPIGA PASAKA CCM MWINYIMKUU PASAKA APRIL 21

Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Hussein Pendeza na Juma Ramadhani 'Choki' wametamba kila mmoja kwa wakati wake juu ya mpambano wao utakaofanyika April 21 siku ya sikukuu ya Pasaka katika ukumbi wa CCM Mwinyimkuu Magomeni Mapipa Dar es salaam

akizungumza kuhusu mpambano wake Juma Ramadhani 'Choki' amesema kuwa kwa sasa yani yupo fit mpaka yeye mwenyewe anajiogopa kutokana na mazoezi anayofanya kwani nimefanya mazoezi ya kutosha na nipo tayali kwa mpambano na yoyote yule sio huyu peke yake bondia yoyote yule alie katika uzito wangu nita akikisha nampiga kipigo cha mbwa mwizi kwa hivyo kaeni chonjo  vinginevyo nitawalalawa laluwa na sijaona katika uzito wangu wa kg 58 wa kunisumbua kwani ninajiamini na nina amini mazoezi ninayo yafanya

Choki amewaomba mashabiki wake wa manzese mabibo pamoja na mbagala kuu na mtoni kijichi wajitokeze kwa wingi kuja kumpa sapoti siku hiyo na wangalie nini anafanya katika mchezo uhu wa masumbwi nchini

nae Pendeza amesema kuwa ata akikisha anampiga kama beg kwa juma ni mtoto mdogo sana katika masumbwi hivyo atajuta kuzaliwa kwa kipigo nitakacho mpatia siku hiyo Pendeza aliongeza kwa kuwaomba mashabiki wake wote na wapenzi wa ngumi kujitokeza siku hiyo kuangalia jinsi anavyo msambalatisha kijana huyo


Mpambano uho ulioandaliwa na Promota wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' amesema kuwa pambano hilo litafanyika siku ya sikukuu ya pasaka likiwa limepewa nguvu na 

Bondia Mtanzania Omari Kimweri 'Lion Boy 'anaefanya shughuli zake nchini Australia  bondia huyo ndie aliesababisha mabondia hawo wazipige siku hiyo kwa kuwa vijana wanatakiwa kuendeleza rekodi zao za masumbwi kila wakati ndio mana akaongeza nguvu ili mpambano uho ufanyike



Super D aliongeza kwa kusema kuwa mbali na pambano hilo siku hiyo kutakuwa na mapambano mbalimbali yatakayokuwa yanafanyika siku hiyo ambapo bondia  Idd Mkwera ataoneshana umwamba na Rojas Masamu na  Shomari Milundi ataoneshana umwamba na Bakari Mbede wakati ibrahimu Makubi atavaana na Haruna Ndalo na Ramadhani Mbegu 'Migwede' atakabiliana na Rashidi Mnyagatwa na Salum Tandu zidi ya Gerald Mkude na Sunday Kiwale 'Moro Best' atalindima na Luckman Ramadhani Vicent Mbilinyi na Shabani Mbogo Hussein Shemdoe na Shehe Azizi na Ahmadi Kombo atakumbana na Sandali Nyambala

Mapambano yote hayo yanaletwa kwenu na kampuni tanzu ya kizalendo ya Super D Boxing Promotion ambayo ipo nchini Tanzania kwa ajili ya kuinuwa vipaji ya vijana mbalimbali ili kuendeleza vipaji vyao pendwa


na kupitia kampuni ya Super D Promotion imejizatiti kuweka angalau pambano moja kila baada ya miezi milili ili kuwasaidia vijana mbalimbali kukuza vipaji vyao na kujiendeleza kupitia mchezo uho wa masumbwi nchini

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.