ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, March 13, 2019

WANAHABARI MWANZA WAPIGWA MSASA KIAFYA ZAIDI.


 Mratibu wa Afya ya Uzazi Wizara ya Afya, Martha Shakinyau(kushoto) akizungumza na Wanahabari jijini Mwanza wakati wa mafunzo ya awali ya namna ya utoaji taarifa kwa jamii juu ya majukwaa mawili yanayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni ya NAWEZA NA SITETELEKI.Kulia ni baadhi ya Wanahabari wa jijini Mwanza wakimsikiliza Mratibu huyo.Mafunzo hayo yalifanyika katika Hotel ya Gold Crest jijini Mwanza.
 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa USAID Tulonge Afya, Prisca Rwezahura(kushoto) akizungumzana Wanahabari jijini Mwanza wakati wa mafunzo ya awali ya namna ya utoaji taarifa kwa jamii juu ya majukwaa mawili yanayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni ya NAWEZA NA SITETELEKI.Kulia ni baadhi ya Wanahabari wa jijini Mwanza wakimsikiliza Mratibu huyo.Mafunzo hayo yalifanyika katika Hotel ya Gold Crest jijini Mwanza.
 Wanahabari wa Jijini Mwanza wakifuatili kwa makini mafunzo yaawali ya namna ya utoaji taarifa kwa jamii juu ya majukwaa mawili yanayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni ya NAWEZA NA SITETELEKI..Mafunzo hayo yalifanyika katika Hotel ya Gold Crest jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.
Wanahabari wa Jijini Mwanza wakifuatili kwa makini mafunzo yaawali ya namna ya utoaji taarifa kwa jamii juu ya majukwaa mawili yanayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni ya NAWEZA NA SITETELEKI..Mafunzo hayo yalifanyika katika Hotel ya Gold Crest jijini Mwanza mwishoni mwa wiki.



Wanahabari Mwanza wapigwa Msasa.

WIZARA ya afya kwa kushilikiana na Mradi wa USAID Tulonge Afya fhi 360  wametoa mafunzo kwa wanahabari jijini Mwanza juu ya utoaji habari wakati wa maandalizi ya uzinduzi wa Majukwaa mawili ya mawasiliano ya afya kwa watu wazima litakaloitwa “NAWEZA” na kwa vijana “SITETELEKI” ili kufikisha elimu sahihi itakayoijengea jamii ya Watanzania uwezo na kubadilisha mitizamo na tabia zao za kiafya na kuleta matokeo chanya.

Mafunzohayoyalifanyikajijini Mwanza mwishonimwa wiki katika Hotel ya Gold Crest ambapo yalipata mwitikio mkubwa na ulewa mzuri kwa wanahabari waishio jijini Mwanza.
Mafunzo hayo yaliendeshwa na wataalamu mambo ya Afya kutoka Wizara ya Afya na USAID Tulonge Afya fhi 360. 

NAWEZA ni jukwaa litakalolenga kuwafikia wananchi tofautitofauti itachangia kuboresha afya na ustawi wa Watanzania wengi, itakuwa ikibadilika badilika ili kukidhi mahitaji ya maeneo mengine ya kiafya muhimu kwa walengwa hao ama makundi mengine hususani watu wazima. 

SITETELEKI ni jukwaa litakalo lenga zaidi kuwafikia Vijana wenye umri kati ya 15 – 24, wanaokabiliwa na changamoto nyingi za malengo ya maisha.



Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.