ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, March 13, 2019

RAIS MAGUFULI ATOA MILIONI MIA SABA UJENZI WA CHUO CHA TAALUMA YA POLISI JIJINI DAR ES SALAAM

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza  na  Askari Polisi  ambao  ni  wanafunzi  katika  Chuo cha Taaluma ya  Jeshi  la  Polisi, wakati  alipotembelea chuoni  hapo  kufuatilia maandalizi  ya awali  baada  ya  jeshi  hilo  kupokea kiasi cha Shilingi Milioni Mia Saba kutoka kwa Rais Dkt. John Magufuli kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho.Ziara hiyo imefanyika  leo jijini Dar es Salaam. Picha  na  Wizara  ya Mambo ya Ndani  ya Nchi
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akitembelea maeneo ya Chuo cha Taaluma ya Polisi  ambacho hivi karibuni kimepokea Shilingi Milioni Mia Saba kutoka kwa Rais Dkt. John Magufuli kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya chuo hicho, kulia ni Mkuu wa Chuo, Naibu  Kamishna, Anthony  Rutashuburugukwa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Naibu  Waziri  wa  Mambo  ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akitembelea maeneo ya Chuo cha Taaluma ya Polisi  ambacho hivi karibuni kimepokea Shilingi Milioni Mia Saba kutoka kwa Rais Dkt. John Magufuli  kwa  ajili  ya  ujenzi  wa majengo ya chuo hicho,Wengine  ni  viongozi wa chuo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na Maafisa wa Jeshi la Polisi wakati wa ziara katika  Chuo  cha Taaluma  ya  Polisi, jijini Dar es Salaam  ambacho hivi karibuni kimepokea Shilingi  Milioni  Mia Saba kutoka kwa Rais Dkt. John Magufuli kwa ajili ya ujenzi wa  majengo  ya  chuo hicho. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi


Masauni aokoa Milioni Mia Mbili za JPM
Na Mwandishi Wetu
Jeshi la Polisi nchini limeelekezwa kutumia wafungwa ili kuweza kuokoa kiasi cha Shilingi Milioni Mia Mbili  kati ya Milioni Mia Saba zilizotolewa na Rais Dk. John Magufuli   katika Mradi wa Ujenzi wa Mabweni na Madarasa ya  Chuo cha Taaluma ya Polisi kilichopo  Kurasini jijini Dar es Salaam.
Maelekezo hayo yametolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni alipotembelea majengo chakavu ya chuo hicho baada ya kupokea kiasi cha Shilingi Milioni Mia Saba alizoahidi Rais Dkt. John Magufuli akihutubia katika mahafali ya kuhitimisha Mafunzo ya Kozi za Uofisa na Ukaguzi Msaidizi  chuoni hapo mwishoni mwa mwaka jana
“Wizara ina taasisi ya magereza ambayo ina nguvu kazi ya kutosha, na Rais alishaagiza wafungwa watumike katika shughuli za uzalishaji, sioni sababu ya kutumia kiasi hicho cha pesa kuwalipa vibarua wa nje, naagiza muwasiliane na Jeshi la Magereza pamoja na kikosi cha ufundi kilichopo ndani ya Jeshi la Polisi ili muweze kuona ni vipi mnaokoa kiasi hicho”alisema Masauni
Akitoa taarifa ya awali ya ujenzi huo, Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi, Naibu Kamishna Anthony Rutashuburugukwa alitaja  majengo yatakayojengwa kuwa ni ghala la chuo, madarasa matatu,bweni moja la askari wa kiume na bweni lingine la askari wa kike.
Wakizungumza kwa masharti ya kutotajwa majina wanafunzi wa chuo hicho walimshukuru Rais Dkt. Johh  Magufuli kwa kiasi cha fedha alichotoa ili kuweza kujenga sehemu mbalimbali za chuo hicho ikiwemo mabweni ambayo wamekiri ni chakavu na si rafiki kwa matumizi ya binadamu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.