Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde (wa pili kushoto) akiwasili kwenye viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma akiwa ameambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko (kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Bi .Mwanahamisi Mukunda (wa pili kulia) pamoja na Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng (kulia) wakielekea kutembelea kijiji cha Vijana wakati wa hafla ya kuhitimisha wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi yayonafanyika Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde akipata maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa kiufundi-FP wa shirika la JHPIEGO, Bi. Lena Mfalila (kushoto) kuhusu shughuli zinazoendeshwa na Shirika hilo kupitia mradi wa Tupange Pamoja (TCI) ambayo ni huduma rafiki ya vijana katika afya ya uzazi kwa vijana wakati walipotembelea kijiji cha Vijana kwenye hafla ya kuhitimisha wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi yayonafanyika Jijini Dodoma. Wengine katika picha ni Mtaalamu wa kiufundi-AYSRH wa shirika la JHPIEGO kupitia mradi wa Tupange Pamoja (TCI), Bw. Waziri Njau (katikati) pamoja na ‘Coacher’ -SRH wa shirika la JHPIEGO kupitia mradi wa Tupange Pamoja (TCI),Bi Rehema Mzungu.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde akipata maelezo kutoka kwa
Mratibu wa Uzazi Salama mkoa wa Dodoma wa Shirika la PSI Tazania, Bi. Sophia
Jamal (kushoto) kuhusu elimu ya afya ya uzazi wanayotoa kwa mabinti kuanzia
miaka 13-19 yenye kauli mbiu ya Binti “Dhamiria kutimiza ndoto yako-“Simama
Imara” “Vaa Taji”, “Kua Mzuri” wakati alipotembelea kijiji cha Vijana kwenye hafla ya kuhitimisha wiki ya
shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani
ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi yanayofanyika katika
viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde na Mkuu wa Wilaya ya Bahi,
Bi .Mwanahamisi Mukunda aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti
Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko wakipata maelezo kutoka kwa Bi.
Debora Frank (kushoto) ambaye ni Afisa Miradi wa Huduma za Vijana wa shirika la EGPAF ambao wanaotekeleza mradi
wa USAID wa Boresha Afya kwa kushirikiana na ENGENDER Health kuimarisha afya za
watanzania wote na kuongeza upatikanaji wa huduma za afya timilifu za kiwango
cha juu na jumuishi wakati alipotembelea kijiji cha Vijana kwenye hafla ya kuhitimisha wiki ya
shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani
ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi yanayofanyika katika
viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma. Mradi unaolenga kuboresha huduma za kinga na
matibabu ya VVU/UKIMWI, uzazi wa mpango, Kifua Kikuu na kutoa huduma mahususi
wa kuyafikia makundi maalum kwa watoto
na vijana.
Pichani ni Hawa Musa (20) mmoja kati ya vijana zaidi ya 2000 wanaonufaika na mafunzo ya ujasiriamali yaliyofadhiliwa na Shirika la EGPAF ambapo mafunzo hayo yamewasiaida kutengeneza bidhaa mbalimbali ikiwemo vikoi, mikoba ya shanga, Ubuyu, sabuni za maji na miche ambazo zinawasaidia kupata fedha za matumizi mbalimbali akishiriki kuonyesha kazi zake katika mabanda ya kijiji cha Vijana wakati wa hafla ya kuhitimisha wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi yanayofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde akipata maelezo kutoka kwa
Meneja masoko wa Shirika lisilo la kiserikali la T-MARC Tanzania, Bi. Sophia
Komba kuhusu shirika hilo linalotoa elimu kuhusu matumizi ya Kondomu ili
kujikinga na maambukizi ya magonjwa ya ngono ikiwa pamoja na UKIMWI katika
mabanda ya kijiji cha Vijana
wakati wa hafla ya kuhitimisha wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha
maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu
inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini
Dodoma. T-MARC Tanzania wanafanya kazi kwa kushirkiana na Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto katika kuboresha afya ya jamii ya
watanzania ambapo pia ni wasambazaji wa bidhaa za afya ambazo ni Kondomu ya
kiume- Dume, Kondomu ya kike Lady Pepeta na vidonge vya uzazi wa mpango-Flexi
P. Wa pili kushoto ni Outreach Educator wa T-MARC Tanzania, Dotto Iddy.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde, Mkurugenzi Mtendaji wa
Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko, Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Bi .Mwanahamisi
Mukunda pamoja na Mkurugenzi
Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS)
nchini, Dk. Leo Zekeng wakipata maelezo kutoka kwa Mshauri mwandamizi wa
masuala ya afya ya uzazi kwa vijana kutoka mradi wa Sauti unaratibiwa na
Shirika la JHPIEGO, Esther Majani (wa kwanza kushoto) kuhusu shughuli
wanazofanya za kutoa elimu ya kupunguza maambukizi mapya ya VVU kwa makundi
hatarishi ikiwemo mabinti walio nje ya shule wa miaka 15-24 wakati
walipotembelea kijiji cha
Vijana kwenye hafla ya kuhitimisha wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele
cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu
inasema Pima Jitambue, Ishi yaliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini
Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Bi .Mwanahamisi Mukunda akizungumza jambo kwa niaba ya Mkuu mpya wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Dkt. Bilinith Mahenge wakati akimkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde akihutubia wananchi wa
Dodoma wakiwemo vijana wakati wa
hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya
Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima
Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.
Balozi wa Vijana ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Mh. Jokate Mwegelo akizungumza na hadhira ya vijana (hawapo pichani) wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko
akitoa neno kwa mgeni rasmi Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,
Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli
za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo
kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja
vya Jamhuri Jijini Dodoma.
Balozi wa Vijana ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe,
Mh. Jokate Mwegelo akibadilishana
mawazo na Mkurugenzi Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la
Umoja wa Mataifa (UNAIDS) nchini, Dk. Leo Zekeng wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli
za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo
kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja
vya Jamhuri Jijini Dodoma.
Msanii wa Bongo Flava Maua Sama akitoa burudani kwa wakazi
wa Dodoma wakati wa hafla ya
kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya
UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue,
Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.
Mchekeshaji maarufu nchini Stan Bakora akitoa burudani ya
kuhamasisha upimaji wa UKIMWI kwa njia ya vichekesho wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli
za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo
kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja
vya Jamhuri Jijini Dodoma.
Afisa Maendeleo Vijana wa Mkoa wa Dodoma, Bw. Tumsifu
Mwasambale (kushoto) akionyesha moja ya picha iliyoshinda wakati wa wiki ya
shughuli za kijiji cha vijana iliyochorwa kijana Edward Malongo na kupigwa
mnada ambapo zaidi shilingi 2.7 zilipatikana ambapo nusu zilienda kwa mchoraji
na nyingine kwenye mfuko wa udhibiti wa Ukimwi (ATF) wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli
za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo
kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja
vya Jamhuri Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde akikabidhi zawadi ya kombe
ya mshindi wa kwanza kwa kapteni wa timu ya mpira ya vijana walio nje ya shule
ya Panama, Bw. Dunia Salumu wakati wa hafla ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha
maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu
inasema Pima Jitambue, Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini
Dodoma.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,
Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mh. Antony Mavunde akikabidhi zawadi ya kombe
ya mshindi wa kwanza kwa kapteni wa timu ya mpira wa pete ya Vijana Queens,
Ngesa Selemani wakati wa hafla
ya kufunga wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku
ya UKIMWI Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue,
Ishi iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.
Pichani juu na chini ni sehemu ya wakazi wa Dodoma
walioshiriki hafla ya kufunga
wiki ya shughuli za vijana kuelekea kilele cha maadhimisho ya Siku ya UKIMWI
Duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi
iliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma.
UNAIDS kuendelea kushirikiana na serikali kupambana na UKIMWI
Na Mwandishi wetu
Mkurugenzi
Mkazi na Mwakilishi wa Shirika la Kupambana na UKIMWI la Umoja wa Mataifa (UNAIDS)
nchini, Dk. Leo Zekeng amesema kuwa kuwa shirika hilo litaendelea
kushirikiana na Serikali katika mapambano dhidi ya Ugonjwa huo.
Akizungumza jana Jijini Dodoma wakati wa kilele cha shughuli
za vijana kuelekea maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani, Dk Zekeng alisema
kwamba kuna haja kubwa ya kuhakikisha kwamba taifa linapambana na maambukizi
mapya kwa kuhakikisha kwamba kunatolewa huduma rafiki miongoni mwa vijana ambao
ndio kundi kubwa linalohitaji msaada kwa sasa ni jukumu la kila mwanajamii na
kuomba ushirikiano wadau wote katika mapambano hayo.
Alisema wakati taifa nusu yake ni vijana wenye umri kati ya
miaka 15-24 na huku takwimu zikionesha kwamba kundi hilo linaathirika sana ipo
kila sababu ya kutengeneza mkakati na kuweka mazingira rafiki ili kuokoa kizazi
hicho.
Alisema kwa sasa vijana wanahitaji kusaidiwa kwa kuwaweka
katika mazingira rafiki ya kuhitaji huduma zinazotolewa katika kampeni ya kukabiliana
na maambukzi ya VVU.
Alisema kwa sasa huduma hizo si rafiki ziko chache na hivyo
kuwafanya vijana wasishiriki kwa sababu ya hofu ya kunyanyapaliwa na pia
kukosekana kwa elimu hitajika.
Aliongeza ili taifa lifikie uchumi wa kati unaotakiwa mwaka
2025 na kufikia agenda 2030 ni lazima liwe ni taifa lenye vijana wanaojitambua
na wenye afya bora.
“iko haja ya kushawishi vijana ambao ndio kundi kubwa
kujitambua na katika package nzima wajue namna ya kujikinga, na kuishi kwa afya
hata kama wana virusi” alisema Dk Zekeng
na kusisitiza kwamba shirika lake litaendelea kushirikiana na serikali
kuhakikisha kwamba vijana wanapatiwa elimu ya kutosha na mahitaji mengine
katika vita dhidi ya UKIMWI.
Alibanisha kuwa takribani watu milioni 37 Duniani wanaishi
na Virusi vya UKIMWI na sehemu kubwa wakiwa katika nchi za Kusini mwa Jangwa la
Sahara.
Siku ya UKIMWI Duniani huadhimishwa kila ifikapo Disemba Mosi
kila mwaka ambapo kauli mbiu ya mwaka huu inasema Pima Jitambue, Ishi ambapo
mwaka huu yanafanyika Jijini Dodoma na Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Warizi Mkuu
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.