ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, November 25, 2018

YANGA YAZIDI KUIACHA SIMBA


Klabu ya Yanga imeweza kusimama kwenye nafasi ya pili kwa kufikisha alama 32 baada ya kuifunga Kagera Sugar mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Uwanja wa Kaitaba, Kagera.

Yanga walikuwa wa kwanza kuandika bao mnamo dakika ya 21 kupitia kwa Mkongoman, Heritier Makambo na baadaye Kagera kusawazisha kwa njia ya tuta ikiwa ni dakika ya 32 kupitia kwa Ramadhan Kapera.

Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza kinamalizika Yanga na Kagera wote walikuwa na mabao sare ya 1-1.

Mnamo kipindi cha pili Yanga walionekana kuongeza kasi na jitihada za kusaka bao la kuongeza na katika dakika ya 74 Raphael Daud alifanikiwa kutikisa nyavu za Kagera kwa njia ya kichwa.

Msimamo wa Ligi hiyo unaonyesha kuwa Azam FC wanashika nafasi ya kwanza kwakua na alama 33, Yanga nafasi ya pili kwa alama 32 na Simba inashika nafasi ya tatu kwakua na alama 27

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.