ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, November 25, 2018

BITEKO ATOA MAAMUZI KILIO CHA WACHIMBAJI WADOGO WA DHAHABU WILAYANI KAHAMA

Na George Binagi-GB Pazzo 
Serikali imesikia kilio cha muda mrefu cha wachimbaji wadogo wa dhahabu katika machimbo ya Bushimangila yaliyopo Halmashauri ya Msalala, Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga kwa kutoa idhini kwa wachimbaji hao kuendelea na shughuli za uchimbaji katika machimbo hayo.

Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko alitoa idhini hiyo jana baada ya kufanya ziara katika machimbo hayo ya Bushimangila kwa lengo la kukagua shughuli za uchimbaji, kusikiliza na kutatua kero za wachimbaji wadogo wa dhahabu.

Awali baadhi ya wachimbaji wadogo wa dhahabu katika machimbo hayo walieleza kufukuzwa na Menan Sanga ambaye anamiliki leseni ya uchimbaji na kuomba serikali kuwapatia leseni ya uchimbaji katika eneo hilo.

Walisema awali eneo hilo lilikuwa likimilikiwa na kampuni ya utafiti ya Lion Town tangu mwaka 1989 na baadaye likakabidhiwa kwa kampuni ya Chela Resources na sasa Menan Sanga na kwamba limekuwa likibadilishwa umiliki kwa muda mrefu bila kuendelezwa huku wao wakitaabika.
 
Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Doto Biteko akizungumza na wachimbaji wadogo wa dhahabu katika Machimbo ya Bushimbangila wilayani Kahama, kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Mhandu.
Mbung wa Jimbo la Msalala, Mhe. Ezekiel Maige akizungumza kwenye mkutano huo na kuelekeza kilio cha wachimbaji wa dhahabu katika machimbo ya Bushimangila.
Tazama Video hapa chini

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.