ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, November 22, 2018

WAFANYABIASHARA MLANGO MMOJA WILAYANI NYAMAGANA WASEMA MBUNGE WAO KAWATOSA



GSENGOtV

MARA baada ya jana Kamanda wa Polisi Mkoani Mwanza, Jonathan Shana kutoa kauli ya ahadi ya kutoa kitita cha shilingi milioni 10 kwa yeyote atakayeweza kuja na picha zakuonesha askari wa jeshi la polisi wakitumia nguvu kuwaondoa wafanyabiashara wa soko la mlango mmoja kwa tukio la jana baada ya sintofahamu ya kufungwa maduka kwa takribani saa kadhaa hii leo Kazi na Ngoma imeona siyo kesi ngoja iliibukie dili hilo.

Awali mapema jana JUMATANO taarifa zilielezwa kuwa wafanyabiashara katika soko la Mlango Mmoja jijini Mwanza wamefanya mgomo ndani ya soko hilo kwa kile walichokidai kuwa Halmashauri ya jiji hilo imeshindwa kuwapatia vibali vya ujenzi wa maduka yao 29 pamoja na vibanda 55 vilivyoteketea kwa moto.

Aidha wafanyabiashara hao wamemgeuzia kibao Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula wakidai kwamba kawatosa kwa kutowapa ushirikiano wa wapigania katika kipindi hiki ambapo hawajui nini hatma yao.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.