Kikosi cha timu ya Yanga kimeweza kuishusha timu Simba na kufikisha pointi 29 baada ya kuwafunga Mwadui FC mabao 2-1 katika mchezo uliochezwa uwanja wa CCM Kambarage.
Na kwamatokeo hayo Yanga wamefanikiwa kuendeleza rekodi yao kwa kucheza michezo 11 bila kupoteza.
Yanga ndiyo waliotangulia kupata bao dakika ya 10 kupitia kwa Heritier Makambo, kabla ya Mwadui kusawazisha dakika ya 40 kupitia kwa Salim Aiyee akitumia makosa ya kipa wa Yanga Klaus Kindoki, lakini mkongwe Mrisho Ngasa akaamua matokeo kwa kuifunga Yanga bao la pili dakika ya 58.
Katika mchezo huu kocha wa Yanga Mwinyi Zahera alilazimika kufanya mabadiliko kwa kumuweka nje kipa Klaus Kindoki na nafasi yake ikachukuliwa na Ramadhan Kabwili, Amissi Tambwe nafasi yake ikachukuliwa na Raphael Daud, na Gadiel Michael nafasi ikachukuliwa na Pato Ngonyani.
Yanga wamecheza leo bila ya kuwa na wachezaji wao kama Ibrahim Ajibu, Kelvin Yondani, Beno Kakolanya na Papy Tshishimbi.
Matokeo haya yanaifanya Yanga kupanda hadi nafasi ya pili ikifikisha pointi 29 katika michezo 11 iliyocheza ambapo imetoka sare michezo miwili na kushinda michezo tisa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.