ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, November 12, 2018

GEITA GOLD V/S PAMBA FC NGUVU SAWA.

Geita gold, Pamba FC zatoka sare
Na James Timber, Geita
TIMU za Geita gold na Pamba FC ya jijini Mwanza zimeshindwa kutambiana baada ya timu hizo kutoka sare ya bao 1-1 katika mchezo wa ligi daraja la kwanza kundi B.

Mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa shule ya sekondari ya wasichana ya Nyankumbu ulishuhudia bao la Pamba FC likifungwa na Ally Rajab katika dk ya 45 kisha wenyeji walisawazisha Bakari Juma dk ya 82.

Kwa upande wake kocha mkuu wa timu ya Geita gold, Hassan Banyai alisema timu yake imecheza vyema tatizo kubwa ni safu yake ya ushambuliaji ilishindwa kutumia nafasi ilizokuwa inatengeneza.

Banyai alisema mchezo ulikuwa mgumu sana kutokana na uwanja haukuwa mzuri kwakuwa wachezaji wake walikuwa wakiteleza muda mwingi.

Kocha huyo wa zamani wa Maji Maji FC na Njombe Mji alisema timu yake ilifanya makosa ,ndipo timu ya Pamba FC ikaweza  kuwaadhibu.

Kocha mkuu wa timu ya Pamba FC Sumbu Juma alisema anashukuru kwa mchezo kumalizika salama licha ya uwanja kuwa mbovu. Alisema lengo lao lilikuwa ni kupata ushindi lakini kwa sare waliopata anawapongeza wachezaji wake.

Pamba FC ndio inayoongoza kundi hilo ikiwa na alama 11 baada ya michezo 6 iliyocheza.Geita gold ipo katika nafasi ya 4 ikiwa na alama 10.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.