ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, November 12, 2018

~LIVE : RAIS DK JOHN POMBE MAGUFULI AKIWAAPISHA MAWAZIRI WATEULE KATIKA UKUMBI WA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amesema, serikali itanunua korosho yote kwa bei ya shilingi 3300/= kwa kilo moja ya isiyobanguliwa.

Mhe. Rais ametoa agizo hilo muda huu baada ya kuwaapisha mawaziri na Manaibu Waziri Ikulu Jijini Dar es Salaam.

"Mimi sio mchumi lakini nimepiga hesabu tani za korosho zilipo nchini tunaweza kuzinunua wenyewe, tena sio kwa bei elekezi 1500 iliyopangwa na Bodi ya Korosho" Mhe. Rais ohn Pombe Magufuli

"Saa zingine tatizo wizara hizi hazishirikiani, sasa muende mkashirikiane na kila Taasisi zilizopo kwenye wizara zenu" Mhe Rais Dkt ohn Pombe Magufuli

"Ili wakulima hawa wapate bei nzuri na wasihangaike, Korosho zao tutanunua kwa bei ya shilingi 3300/= kwa kilo. Hawa wakulima ndio waliotupigia kura, sasa korosho zao, tunataka wakulima wetu wasipate shida ndio ahadi tulioitoa" Mhe Rais Dkt ohn Pombe Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt ohn Pombe Magufuli ameihamishia ofisi ya Waziri Mkuu Kituo Cha Uwekezaji (TIC) kwa kile alichokieleza kuwa idara hiyo kuingiliwa, lakini pia ikiwa chini ya Ofisi Waziri Mkuu itakuwa rahisi kwake kuangalia mwenendo wa idara hiyo.

"Kuna wanasiasa wengine ndio wanaowatuma watu wao kule kununua korosho kwa mtindo wa 'Kangomba', halafu wanasiasa hao ndio wasemaji na wanapiga kelele kuhusu korosho, wanafikiri sisi tumekaa kimya kanakwamba hatulijui hilo" Mhe Rais. Dkt ohn Pombe Magufuli

"Tuna kila kitu lakini tunakuwa tunaogopa ogopa kuchukua maamuzi magumu, kwa mwenendo huu wa sekta binafsi hapa nchini kuingiliwa na kufanya kazi isiyofaa, serikali itaendelea kuchukua hatamu" Mhe Rais Dkt ohn Pombe Magufuli

"Kuna wabunge kama watano hivi kazi yao ni kukaa na kuwaza uwaziri tu, na mimi nimeshawaweka pembeni huko muda mrefu" Mhe Rais Dkt ohn Pombe Magufuli

"Hizi bodi zingine sasa zianze kutafuta na mazao mengine, lakini katika hili nataka TIC ambayo huko iliko haifanyi vizuri, sasa ihamie kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu ili iratibu uwekezaji kwa wizara zote" Mhe. Rais Dkt ohn Pombe Magufuli

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.